If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Saturday, July 8, 2017

RAIS KENYATTA AMTEUA MATIANG'I KUWA KAIMU WAZIRI WA USALAMA

Na CHARLES WASONGA

RAIS Uhuru Kenyatta Jumamosi saa nne asubuhi, amemteua Waziri wa Elimu Dkt Fred Matiang'i kuwa kaimu Waziri wa Usalama wa Ndani. Hii ni kufuati kifo cha ghafla cha Meja Jenerali Mstaafu Joseph Ole Nkaissery usiku wa kuamkia Jumamosi huku akitoa hakikisho kwamba usalama wa taifa ni thabiti.

Fred Matiang'i
Waziri wa Elimu Dkt Fred Matiang'i. Rais Kenyatta amemteua Julai 8, 2017 kusimamia Wizara ya Usalama wa Ndani kufuatia kifo cha Meja Jenerali Mstaafu Joseph Nkaissery. Picha/MAKTABA

Akihutubia taifa katika Ikulu ya Nairobi Rais aliwataka Wakenya kuwa watulivu wakati huu wa maombolezi akisema vikosi vya usalama viko imara kudumisha usalama wa ndani na kulinda mipaka ya Kenya.

"Kifo cha Waziri Nkaissery kimejiri wakati ambapo taifa hili linajiandaa kwa Mashindano ya Kimataifa ya Riadha ya Vijana na wakati ambapo taifa hili pia linajiandaa kwa uchaguzi mkuu. Lakini ningependa kuhakikishia Wakenya kuwa usalama nchini bado uko thabiti," akasema Rais Kenyatta.

Akaendelea: "Leo asubuhi nimeongoza mkutano wa baraza la usalama na ili kuhakikisha kuwa hamna pengo katika usimamizi wa usalama nchini nimemteua Waziri wa Elimu Dkt Fred Matiang'i kuwa Kaimu Waziri wa Usalama wa Ndani".


Rais alituma risala za rambirambi kwa jamaa na marafiki wa marehemu Nkaissery akisema serikali yake na taifa kwa jumla imempoteza Waziri mchapakazi aliyejitolea katika majukumu yake.

"Kwa hivyo, nawaomba Wakenya kuwa watulivu wakati huu wa majonzi. Tutawajulisha kuhusu kifo chake baadaye Jumamosi baada ya mwili wa marehemu kufanyiwa upasuaji," akasema Rais Kenyatta ambaye alikuwa ameandamana na mawaziri kadhaa akiwemo Waziri wa Ulinzi Bi Rachel Omamo.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako