If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Friday, July 7, 2017

Tanzania yahitaji wafanyakazi zaidi ya elfu 7 wa afya kuziba pengo

Serikali ya Tanzania imeombwa kutoa kibali cha dharura cha kuajiri watumishi 7,304 ambao ni madaktari, manesi na wahudumu wa afya baada ya watumishi takribani 3,439 kukumbwa na sakata la vyeti feki na kuacha zahanati 285 zikiwa hazina mtumishi mwenye ujuzi na hIvyo vituo vya huduma 1,505 kukosa waganga watabibu.

Ombi hilo limetolewa na maofisa wa matibabu wa kikanda nchini Tanzania ambao wameitaka serikali ya nchi hiyo kuwaajiri haraka wafanyakazi 7,304 wapya wa afya ili kuziba pengo lililoachwa na wafanyakazi waliofukuzwa kazini kutokana na vyeti feki.

Mwenyekiti wa maofisa wa matibabu wa kikanda Tanzania Bara, Bw. Lenonard Subi amesema kuwa, wafanyakazi zaidi ya elfu 7 wanatakiwa kuajiriwa kabla ya hali za hospitali haijawa mbaya na kushindwa kudhibitika.

Hospitali ya Mwananyamala

Akizungumza kwenye mkutano huo unaoendelea kufanyika mkoani Dodoma, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk Laurean Ndumbaro alisema wiki ijayo watatoa vibali 3,000 vya ajira katika sekta ya afya ikiwemo vya madaktari, wauguzi na maofisa hesabu 535 kwa ajili ya vituo vya afya vya kata ili washughulike na ukusanyaji wa mapato kwenye vituo vya afya na zahanati.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Mpoki Ulisubisya alisema serikali itaendelea kuajiri watumishi katika sekta ya afya. Alisema kila mkoa umepata mgawo wa madaktari 258 ambao walikuwa wamesailiwa kwenda kufanya kazi nchini Kenya.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako