If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Tuesday, July 4, 2017

Trump: Ni lazima China ichukue hatua kali dhidi ya Korea Kaskazini

Rais Donald Trump wa Marekani ameitaka Uchina kuchukua uamuzi mgumu kuhusiana na hatua ya Pyongyang ya kuvurumisha kombora jipya la balestiki mapema leo.

Kufuatia hali hiyo Trump ameitaka Beijing kuchukua hatua kali kukabiliana na Korea Kaskazini. Kupitia ujumbe aliouandika katika akaunti yake ya Twitter Trump amesema kuwa, ni suala lisilowezekano kwa Japan na Korea Kusini kuweza kuvumilia hatua alizozitaja kuwa eti za uchochezi za Korea Kaskazini. 

Asubuhi ya leo Korea Kaskazini imevurumisha kombora jipya la balestiki katika kutoka katika eneo la ardhi yake lililo karibu na mpaka wa Uchina kuelekea bahari ya Japan.

Kim Jong-un, Kiongozi wa Korea Kaskazini akifuatilia zoezi

Kufuatia hatua hiyo, Tokyo imetangaza kuwa, kombora hilo la Korea Kaskazini limetia doa uchumi wake. Uvurumishaji wa kombora hilo umefanyika zikiwa zimepita siku chache tangu Trump akutane na Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini mjini Washington ambapo walijadili masuala mbalimbali hususan Korea Kaskazini. 

Weledi wa mambo wanaamini kuwa, siasa za uhasama za Marekani kuilenga Pyongyang ndizo zimeifanya Korea Kaskazini izidi kujiimarisha kijeshi kwa kuboresha makombora yake ya balestiki na silaha zake za nyuklia. 

Katika hatua nyingine Baraza la Usalama wa Taifa la Korea Kusini, limeitisha kikao cha dharura kwa ajili ya kujadili kitendo cha Korea Kaskazini cha kuvurumisha kombora jipya la balestiki mapema leo.

Kim Jong-un

Katika kikao hicho Rais Moon Jae-in ameonyesha masikitiko yake juu ya hatua hiyo ya Pyongyang huku akitaka kuchukuliwa hatua thabiti kwa ajili ya kukabiliana na nchi hiyo jirani aliyoitaja kuwa hasimu. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, viongozi wa ngazi ya juu wa Ulinzi, kijeshi, kiusalama na washauri wa rais kwa pamoja wamejadili suala hilo. Inaelezwa kuwa, kombora hilo lililovurumishwa na Pyongyang limeenda umbali wa kilometa 930.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako