If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Saturday, July 1, 2017

UN yaafiki kupunguza bajeti ya wanajeshi walinda amani kwa mashinikizo ya USA

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limekubali kupunguza kwa kiasi kikubwa bajeti ya operesheni za kulinda amani kufuatia mashinikizo ya Marekani.

Kamati ya Bajeti ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana usiku iliidhinisha bajeti ya dola bilioni saba na milioni mia tatu kwa ajili ya oparesheni 14 za askari jeshi wa kulinda amani katika kipindi cha mwaka huu unaoanzia tarehe Mosi Julai. Kiwango hicho cha pesa kimekubaliwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa baada ya kufanyika mazungumzo marefu na mijadala chungu nzima.

Wanajeshi wa kofia bluu wa UN wakiwa katika oparesheni za kudumisha amani

Bajeti ya oparesheni za wanajeshi wa Kofia Bluu mwaka 2016 ilikuwa ya dola bilioni 7 na milioni 870 ambapo sasa imepunguzwa na kufika dola bilioni saba na milioni mia tatu baada ya kupunguzwa kiasi cha dola milioni 570.

Serikali ya Rais Donald Trump wa Marekani ilifanya kila iwezalo kufanikisha zoezi la kupunguzwa bajeti ya vikosi vya askari wa kulinda amani duniani na ilitaka bajeti hiyo ipunguzwe kwa asilimia 13. Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Stephen Dujaric ameeleza kuwa, kiujumla bajeti hiyo ni ya chini kulinganisha na ya mwaka uliopita. Hata hivyo amesema umoja huo utafanya kila uwezalo ili oparesheni za kulinda amani zitekelezwe.

Chanson: parstoday.com

1 comment:

  1. Wanajeshi wetu lazima wapewa motisha ya kufanya kazi licha ya matatizo magumu yaliyoko

    ReplyDelete

Maoni yako