If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Friday, July 7, 2017

Viongozi wamtenga Trump katika mkutano wa G20

Na Daniel Gakuba

Mkutano wa kilele wa G20 umeendelea kwa faragha mjini Hamburg huku kukiwa na taarifa kuwa viongozi wote wamemtenga rais wa Marekani Donald Trump kuhusu upinzani wake kwa mkataba wa mazingira wa Paris.

G20 Gipfel in Hamburg | Trump & Jinping & Merkel (Reuters/K. Nietfeld)
Kansela Angela Merkel (kulia) Xi Jimping na Donald Trump wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kilele wa G20

Katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo mapema leo, mwenyeji, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amewatolea wito wenzake kufikia maridhiano kuhusu masuala ya biashara na mabadiliko ya tabia nchi, ambapo Rais wa Marekani amejikuta peke yake, dhidi ya karibu viongozi wengine wote wanaokutana.

Bi Merkel amewakumbusha viongozi hao kuwa mamilioni ya watu kote duniani wanafuatilia kinachoendelea katika mkutano huo, wakiwa na matumaini kuwa changamoto na hofu zao zitapatiwa ufumbuzi. Amesema kundi lao linawakilisha maslahi ya eneo kubwa la dunia, na kuongeza kuwa hata wale ambao viongozi wao hawamo ndani ya chumba cha mkutano huo, wanategemea maamuzi mazuri.

''Ni sahihi kabisa kwa wale ambao hawapo hapa kutarajia kuwa tutafanya kazi nzuri. Tumejaribu ipasavyo, na kwa upande wa Ujerumani, tumeweka agenda kuhusu masuala ya uchumi na sera zinazohusu mazingira na nishati.'' amesema Merkel na kuongeza kuwa Ujerumani imeiangazia Afrika, kwa sababu bara hilo ni jirani ambayo Ulaya itafanya vyote iwezavyo kumsaidia kusonga mbele.

Trump asababisha utata, ajikuta akitengwa

Deutschland Hamburg - G20 - Donald Trump
Sera za Rais Trump kuhusu mabadiliko ya tabianchi imemweka katika hali ya kutengwa

Bi Merkel ambaye anakabiliwa na uchaguzi mkuu mwezi Septemba, anakabiliwa na kibarua kigumu kuweza kupata muafaka katika mkutano, kuhusu masuala ya biashara, mazingira na wahamiaji, ambayo yamekuwa yenye mvutano mkubwa tangu Trump alipoingia madarakani.


Shirika la habari la China Xinhua limeripoti kuwa rais wa nchi Ji Xinping ameungana na Kansela Merkel, katika kutaka makubaliano kuhusu uhuru wa biashara, na kuzingatia ulinzi wa mazingira katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.

Katika tangazo lao la pamoja muda mfupi kabla ya mkutano huo kufunguliwa rasmi, viongozi wa kundi la nchi 6 zinazoinukia kiviwanda lijulikanazo kama Brics, ambazo ni Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini, zimetaka pia kuheshimiwa kwa mkataba wa mabadiliko ya tabia nchi wa Paris, ambao utawala wa Trump umeamua kutouunga mkono.

Soma zaidi: dw.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako