If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Thursday, July 13, 2017

Wacanada waandamana kupinga ziara ya familia ya Trump katika mji wa Vancouver

Wakazi wa mji wa Vancouver, Canada wamefanya maandamano makubwa kupinga ziara ya familia ya Rais Donald Trump wa Marekani katika mji huo.

Maandamano hayo yamefanyika baada ya baadhi ya watu wa familia ya Rais Trump, kuwasili mjini Vancouver kwa minajili ya kufungua hoteli mpya iliyopewa jina la 'Trump' na kulaani vikali ujio wa watu wa familia ya rais huyo anayepingwa kila kona ya dunia. Gazeti la Washington Post limeandika kuwa, katika ufunguzi wa hoteli hiyo, walifika watoto wawili wa kiume na binti ya rais huyo wa Marekani mjini hapo Vancouver.

Vijana wawili na mabinti wa Rais Donald Trump

Gazeti hilo limewataja watoto hao kuwa ni 'Eric Trump' na 'Donald Trump Jr' watoto wawili wa kiume wa Trump na 'Tiffany Trump' binti mwingine wa Trump na kwamba watoto hao waliambatana na wake na waume zao chini ya ulinzi mkali. 

Baada ya kujulikana ujio wa watu wa familia ya rais huyo, wakazi wa Vancouver walikusanyika kwa wingi na kufanya maandamano ambayo yaliishia mbele ya jengo la hoteli waliyoenda kuifungua huku wakitoa nara zinazosema 'Watu wa Trump waondoke nchini kwetu.' 

Baada ya Rais Trump kuingia madarakani nchini Marekani watoto wake ndio waliochukua jukumu la kupanua harakati za kiuchumi za familia ya Trump huku wakifanya safari katika nchi mbalimbali za dunia zikiwemo Uruguay, Ireland na Imarati.

Sehemu ya jumbe za maandamano hayo

Hata hivyo kwa kawaida harakati hizo za kiuchumi zimekuwa zikipingwa vikali hata ndani ya Marekani kwenyewe. Wapinzani wanasema kuwa, harakati hizo zinatia wasi wasi mkubwa kutokana na utumiaji mbaya wa madaraka wa Rais Donald Trump na watu wake wa karibu ambapo anapanua wigo wake wa kiuchumi kupitia madaraka ya kisiasa aliyonayo hivi sasa.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako