If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Saturday, July 22, 2017

WAKIMBIZI KUTOKA BURUNDI WALIO TANZANIA WASHAURIWA KURUDI KWAO

Na LAWRENCE ONGARO

WAKIMBIZI kutoka Burundi walioko nchini Tanzania wameshauriwa kurejea kwao ili kusaidia kwa ujenzi wa taifa lao.

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza akihutubu baada ya kuapishwa kuongoza taifa hilo kwa muhula wa tatu ikulu ya Congress, mtaa wa Kigobe mjini Bujumbura Agosti 20, 2015. Picha/AFP

Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli alitoa mwito huo baada ya rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza kuzuru Tanzania wiki hii na kuwarai raia wa Burundi ambao ni wakimbizi wakubali kurejea nyumbani ili wamsaidie kwa ujenzi wa taifa hilo la Burundi.

"Nyinyi Warundi mlio hapa mnastahili kurejea nyumbani ili msaidie kwa ujenzi wa taifa lenyu. Kwa wakati huu nchi imetulia na rais wenyu yupo hapa kwa madhumuni hayo," alinukuliwa Bw Magufuli, akisema juzi katika kituo cha wakimbizi cha Ngara katika mpaka wa Burundi na Tanzania.

Rais Nkurunziza alichaguliwa kwa mara ya tatu kama rais wa Burundi ambapo wakazi wengi hawakufurahishwa na jambo hilo huku wengi wakitoroka kutokana na vurugu zilizoshuhudiwa Julai 2015 baada ya Bw Nkurunziza kuapishwa kwa mara ya tatu kama rais.

Kwa muda wa miaka miwili hivi uhusiano wa nchi hizo mbili haujakuwa wa kuridhisha lakini wakati huu uhusiano umerejea na kuwa shwari.

Nkurunziza aliwahakikishia usalama wao wakimbizi wa Burundi walio nchini Tanzania.


"Ninawahimiza Warundi wenzangu mrejee nyumbani ili tuweze kujenga taifa letu changa," alisikika akiyasema hayo alipozuru nchini Tanzania wiki hii.

Kulingana na ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa, kwa muda wa miaka miwili iliyopita wa Burundi wapatao 2,000 tayari wamepoteza maisha yao kwa kuuawa kwa kuikashifu serikali ama wakitorokea usalama wao.

Hata hivyo wengi wa wakimbizi hao wanahofia maisha yao iwapo watarejea katika nchi yao ya kuzaliwa, licha ya kupewa hakikisho kuwa mambo ni shwari kwa wote.

Inadaiwa wakimbiza wapatao 240,000 walikuwa wametafuta hifadhi katika nchi ya Tanzania kwa muda wa miaka miwili iliyopita.

Chanzo: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako