If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Sunday, July 9, 2017

Wanasiasa wawili kuchuana na Kagame katika uchaguzi wa rais Rwanda

Rais Paul Kagame wa Rwanda anatarajiwa kuchuana na wanasiasa wawili katika uchaguzi wa mwezi ujao wa Rais nchini Rwanda, huku duru mbalimbali zikimtabiria ushindi mkubwa.

Hiyo ni baada ya Tume ya Uchaguzi nchini Rwanda, kuwaidhinisha wagombea wawili wa upinzani kupambana na rais Paul Kagame wakati wa Uchaguzi Mkuu mwezi ujao, baada ya wagombea wengine akiwemo mwanamke pekee kushindwa kukamilisha masharti.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Tume ya Uchaguzi ya Rwanda Profesa Kalisa Mbanda ni kuwa kuwa, wanasiasa hao wawili wa upinzani waliokidhi vigezo vya kuwania urais ni pamoja na Frank Habineza, kutoka chama cha Democratic Green Party na mgombea binafsi Philippe Mpayimana.

Rais Paul Kagame anayepewa nafasi kubwa ya kushinda kiti cha uraias katika uchaguzi wa mwezi ujao nchini Rwanda

Taarifa zaidi zinasema kuwa, Gilbert Mwenedata, Fred Barafinda Skikubo na mwanamke wa pekee Diane Rwigara hawakufanikwia kuidhinishwa baada ya kushindwa kupata saini 600 za wapiga kura kama inavyotakiwa kikatiba.


Hayo yanajiri katika hali ambayo, kampeni rasmi za uchaguzi huo, zinatarajiwa kuanza tarehe 14 mwezi huu na kumalizika Agosti tatu ikiwa ni siku moja kabla ya kufanyika uchaguzi wenyewe.

Duru za kieneo na kimataifa zinamtabiria ushindi mkubwa Rais Kagame katika uchaguzi huo wa mwezi ujao hasa kutokana na kutokuweko upinzani mkali. Hatau ya baadhi ya wapinzani kutangaza kumuunga mkono Rais Kagame imepelekea kudhoofika upinzani na hivyo kukiandalia chama tawala cha RPF fursa ya kuendelea kutawala nchini humo.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako