If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Thursday, July 6, 2017

Watu 12 wauawa katika mapigano ya hivi karibuni DRC

Watu 12 wameripotiwa kuuawa katika mapigano ya hivi karibuni kabisa baina ya waasi na jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika mkoa wenye machafuko wa Kivu Kusini, mashariki mwa nchi hiyo kubwa na pana ya katikati mwa Afrika.

Shirika la habari la AFP limemnukuu msemaji wa jeshi la Kongo katika jimbo la Kivu Kusini, Kepteni Dieudonne Kasereka akisema kuwa, mapigano hayo yametokea baina ya waasi wa Mai Mai na askari wa serikali na kupelekea kuuawa wanajeshi wawili na waasi tisa pamoja na raia mmoja.

Kepteni Kasereka ameongeza kuwa, kuna uwezekano wa kuongezeka idadi ya wahanga wa mapigano hayo ambayo yametokea katika eneo linalodhibitiwa na waasi wa Mai Mai. Wanachama wanne wa waasi hao wametiwa mbaroni na jeshi la serikali ambalo limefanikiwa pia kupata silaha nzito kutoka katika eneo hilo lililokuwa linadhibitiwa na waasi.

Waasi wawili wa Mai Mai wakiwa nje ya kibanda katika kijiji cha Kalenge, mashariki mwa DRC


Mapigano makali yamezuka tangu siku chache zilizopita baina ya wanajeshi wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na waasi wa Mai Mai, mashariki mwa nchi hiyo.

Taarifa zinasema kuwa kuna makundi kadhaa ya waasi wa kabila la Mai Mai katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Maafisa wa jeshi la nchi hiyo aidha wamekiri kuwa, waasi wa Mai Mai wamefanikiwa kuteka sehemu nne za eneo la Fizi zilizokuwemo mikononi mwa jeshi la serikali.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako