If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Saturday, July 8, 2017

Waziri wa Usalama wa Ndani wa Kenya Joseph Nkaissery afariki dunia

Waziri wa Usalama wa Ndani wa Kenya amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali moja mjini Nairobi.

Taarifa zaidi zinasema kuwa, Nkaissery amefariki dunia katika Hospitali ya Karen mjini Nairobi. . Waziri Nkaissery alifariki dunia saa chache baada ya kulazwa ghafla katika hospitali ya Karen jijini Nairobi.

Kifo cha Nkaissery kimewashtua Wakenya waliomkia habari hii mbaya siku hii ya Jumamosi.

Mara ya mwisho kuonekana hadharini ilikuwa ni siku ya Ijumaa wakati wa maombi ya wagombea urais katika bustani ya Uhuru jijini Nairobi na kuonekana kuwa mwenye afya.

Kifo hiki kimetokea siku 30 kamili kuelekea Uchaguzi Mkuu nchini Kenya baadaye mwezi ujao.

Marafiki na familia baada ya kupata habari ya kifo cha Waziri Nkaissery

Nkaissery aliteuliwa kuwa Waziri wa Usalama wa Ndani wa Kenya mwaka 2014 akitokea chama cha upinzani cha ODM akimrithi Joseph Ole Lenku.

Kati ya mwaka 2008-2013 alikuwa Naibu Waziri wa Ulinzi katika serikali ya muungano.

Alikuwa mbunge wa zamani wa upinzani jimbo la Kajiado ya Kati kwa miaka 12.

Hadi sasa hakujatolewa taarifa kuhusiana na kilichosababisha kifo cha waziri huyo wa usalama wa ndani wa Kenya.

Jenerali Nkaissery amefariki siku chache baada ya mwanasiasa mkongwe Godfrey Gitahi Kariuki aliyekuwa seneta wa jimbo la Laikipia kufariki dunia.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako