If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Saturday, August 12, 2017

Hatimae Uhuru Kenyatta atangazwa rasmi mshindi wa uchaguzi wa rais wa Kenya

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya IEBC imemtangaza rasmi Rais Uhuru Kenyatta mshindi wa uchaguzi wa rais uliofanyika siku ya Jumanne ya tarehe 8 Agosti.

Akitangaza matokeo hayo mnamo saa nne usiku jana mwenyekiti wa EBC Bw Wafula Chebukati alisema: "Ninachukua fursa hii kumtangaza mheshimiwa Uhuru Kenyatta kuwa Rais wa tano wa Jamhuri ya Kenya akisaidiwa na mgombea mwenza William Ruto kama Naibu Rais".

Chebukati alitoa tamko hilo baada ya kutangaza matokeo rasmi ya uchaguzi wa rais ambayo yameonyesha kuwa Uhuru Kenyatta aliyegombea kwa tiketi ya chama cha Jubilee alipata ushindi baada ya kujizolea kura 8,203,290 sawa na asilimia 54.27 ya kura zote huku mshindani wake mkuu Raila Odinga wa muungano wa upinzani wa NASA akipata kura kura 6,762,224 sawa na asilimia 44.74 ya kura zote.

Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati

Kwa matokeo hayo, Rais Uhuru Kenyatta wa mrengo wa Jubilee na Naibu wake William Ruto wataongoza tena Jamhuri ya Kenya kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Akihutubia mara baada ya kutangazwa mshindi na kukabidhiwa cheti cha kuchaguliwa, Rais mteule Uhuru Kenyatta ameomba Wakenya wadumishe amani na kushirikiana na serikali yake kukuza taifa hilo.

Muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi, Kenyatta alifululiza hadi katika ukumbi wa KICC jijini Nairobi ambapo alihutubia taifa na kumshauri kinara wa Nasa Raila Odinga kwamba uchaguzi huo ulikuwa mashindano tu na haufai kuleta chuki.

Uhuru Kenyatta (kushoto) na mgombea wake mwenza William Ruto mara baada ya kukabidhiwa cheti cha kuchaguliwa Kiongozi huyu aidha amesema atahudumia kila Mkenya bila ubaguzi wowote.

Hayo yanajiri huku muungano wa upinzani wa NASA ukiyakataa matokeo ya uchaguzi na kusisitiza kuwa zoezi hilo lilikumbwa na wizi wa kura.


Licha ya kusema kuwa inapinga matokeo hayo, NASA imesisitiza kuwa haitaelekea mahakamani kukata rufaa na hadi sasa haifahamiki iwapo itabadilisha mawazo yake na kutaka haki katika idara ya mahakama au la.

Wakati huohuo ripoti kutoka Nairobi zinaeleza kuwa polisi wamelazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi kudhibiti malalamiko ya kisiasa yaliyoibuka katika mji wa Kisumu magharibi mwa Kenya iliko ngome kuu ya upinzani na pia katika eneo al mabanda la Mathare katika mji mkuu wa nchi hiyo.

Malalamiko na machafuko hayo yalizuka muda mchache baada ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC kumtangaza Rais Kenyatta mshindi wa uchaguzi wa rais…/

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako