If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Wednesday, August 9, 2017

Kenyatta anaongoza katika matokeo ya uchaguzi Kenya

Matokeo ya mwanzo ya uchaguzi mkuu wa Kenya yanaendelea yanayonesha kuwa Rais Uhuru Kenyatta anaongoza na pengo kubwa dhidi ya mpinzani wake mkuu Raila Odinga.

Kenia Wahlen Präsident Uhuru Kenyatta bei Stimmabgabe (picture-alliance/abaca/A. Wasike)
Kenia Wahlen Präsident Uhuru Kenyatta bei Stimmabgabe (picture-alliance/abaca/A. Wasike)
Mgombea wa uchaguzi wa rais kwa tikiti ya muungano wa upinzani – NASA Raila Odinga ameyakataa matokeo yaliyotolewa mpaka sasa akisema tume ya uchaguzi inahitajika kisheria kuonyesha fomu zilizotiwa saini na waangalizi wa vyama kutoka kila kituo cha kupigia kura zikiidhinisha matokeo kitu ambacho hakijafanyika. "Fomu namba 34 hazipoaswi kuja baada ya matokeo. 

Zinapaswa kuandamana na matokeo. Hivyo tunakataa matokeo yote yaliyotangazwa mpaka sasa, na tunataka IEBC itoe fomu namba 34 kutoka vituo vyote kabla matokeo mengine yote hayajatangazwa" amesema Raila

Badala yake, tume hiyo ya uchaguzi inamwonyesha kwenye tovuti yake, Rais Uhuru Kenyatta akiwa kifua mbele na asilimia 55 ya kura dhidi ya Odinga ambaye ana asilimia 44 baada ya karibu robo tatu ya vituo vya kupigia kura kuwasilisha matokeo yao.

Kenia Raila Odinga PK in Nairobi (Reuters/B. Ratner)

Kenia Raila Odinga PK in Nairobi
Odinga anasema matokeo yanayotolewa sio ya kweli

Hata hivyo, tume hiyo haijatoa habari kuhusu ni majimbo gani yaliyohesabiwa, hivyo haikuwa wazi kujua kama ngome za wafuasi wa Kenyatta au za upinzani, au kutoka pande zote mbili zimehesabiwa au la. 

Odinga anapinga tarakimu hizo akisema uongozi wa Kenyatta umezusha shaka kwa kuwa umebaki pale pale tangu zoezi la kujumlisha kura lilianza na haziendani na kile ambacho anaambiwa na mawakala wa chama chake ambazo zinaonyesha kuwa wako kifua mbele. 

Lakini upande wa chama cha Jubilee umepinga kauli ya NASA ukisema muungano huo unakwenda kinyume na uamuzi uliotolewa na mahakama baada ya wao wenyewe kuwasilisha kesi mahakamani wakitaka matokeo yanayotangazwa katika kituo cha kupigia kura yawe ndiyo ya mwisho. 

Raphael Tuju ni Katibu Mkuu wa chama cha Jubilee "Tunaona wao sio wakweli. Kwa wao sasa kubadilisha msimamo wao. Sidhani kama unaweza kubadilisha sharia wakati mchakato ukiendelea. Sheria ni sheria na lazima sote tuziheshimu"

No comments:

Post a Comment

Maoni yako