If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Monday, August 21, 2017

Mkuu wa Ofisi ya Baraza la Mahusiano ya Kiislamu US akosoa matamshi ya kibaguzi ya Trump

Mkuu wa Ofisi ya Baraza la Mahusiano ya Kiislamu nchini Marekani katika eneo la kaskazini mwa jimbo la Texas amekosoa vikali matamshi ya Rais Donald Trump wa nchi hiyo katika kuunga mkono kundi la wazungu wanaojikweza na kujiona bora kuliko watu wengine.

Alia Salim ambaye alishiriki katika maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi mjini Dallas amewahutubia washiriki wa maandamano hayo kwa kusema kuwa, raia wa Marekani hawataki kuwaona watu wenye fikra za kibaguzi ambao wanaushambulia mkusanyiko wa amani wa waandamanaji kisha kitendo hicho kusifiwa na rais. 

Akiashiria tukio la tarehe 12 ya mwezi huu huko katika jimbo la Virginia ambapo kijana mmoja wa kundi la wazungu wanaojikweza aliwashambulia watu waliokuwa wakiandamana kupinga ubaguzi wa rangi nchini humo na kusababisha mwanamke mmoja kuuawa na wengine 19 kujeruhiwa.

Maandamano ya kupinga ubaguzi Marekani

Katika radiamali ya kitendo hicho, Rais Donald Trump alitoa matamshi yenye kuunga mkono upande wa kundi la kibaguzi kwa kuyataja makundi yote mawili, yaani lile la wazungu na wale wanaopinga ubaguzi kuwa wote ni wakosa. 


Alia Salim sambamba na kutaka kuheshimiwa hisia na harakati za watu wanaopinga ubaguzi amesisitiza kuwa, Wamarekani hawana mazungumzo yoyote na wazungu hao wanaojiona bora na kwamba, kamwe hakutakuwa na mazungumzo baina yao. 

Maelfu ya raia wa Marekani wamekuwa wakifanya maandamano katika miji mbalimbali ya nchi hiyo kupinga sera za kibaguzi za wazungu.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako