If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Friday, August 11, 2017

MOHAMED ALI WA JICHO PEVU ACHAGULIWA MBUNGE WA NYALI

Na MWANGI MUIRURI

MACHI , 2017, mtandao wa Swahilihub ulikufichulia habari kwamba mwanahabari mpekuzi wa runinga ya KTN Bw Mohamed Ali wa kuandaa makala yake ya Jicho Pevu alikuwa amejiuzulu kazini na kujiunga na siasa.

Mohamed Ali
Mwaniaji aliyeshinda ubunge eneobunge la Nyali, Mohamed Ali aliyeikacha kazi ya uanahabari wa upekuzi wa Jicho Pevu runinga ya KTN ahutubu Machi 21, 2017 katika Orange House jijini Nairobi. 

Hii ni baada ya makala hayo yake kukosa kupeperushwa kwa wiki tatu mfululizo, kiasi kwamba kulikuwa kumezuka taharuki miongoni mwa mashabiki wake kuwa huenda alikuwa amekumbana na hatari ya kuangazia mafisadi na majambazi wa kila aina.

Ni wakati Swahilihub ilipata kwa mitandao ya kijamii udaku kuwa Ali alikuwa ametoweka, ikidaiwa pia alikuwa ametekwa nyara ambapo tulipekua na kupata ukweli wa mambo kuhusu kujiunga kwake na siasa katika eneobunge la Nyali, Kaunti ya Mombasa.

Baada ya kutesa nyanjani akisaka uungwaji mkono, akiwa mfuasi wa chama cha Orange Democratic Movement lakini akaibuka na ushindwe katika kura ya mchujo wa chama hicho.

Alilia kuwa alikuwa amechezewa ngware kisiasa, akajaribu kujitetea katika makao makuu ya ODM lakini akakosa wa kumpa afueni.

Ndipo alijiunga na mrengo wa wawaniaji wa kujitegemea na akajipata katika debe la kura kuu Agosti 8, 2017. Kilicho chako ni chako hata iweje, sasa ni tabasamu kuu kwa Ali kwa kuwa ndiye mbunge mpya wa Nyali.


Anarithi majukumu ya Hezron Awiti ambaye aliamua kuwania ugavana Mombasa dhidi ya Ali Hassan Joho lakini ikawa ndiyo kujikwaa kwake ambapo Joho alivuka mstari wa ushindi kabla ya wote washindani wake waelewe mbinu zake.

Akiwania kama Mohamed Ali Mohamed, amepata ushindi wa asilimia 43.75 ya kura zilizopigwa Nyali, akimlemea Said Abdala Salim aliyezoa asilimia 26.69, akiwa ndiye alikuwa amepewa tiketi ya ODM dhidi ya Ali.

Matokeo hayo yanaonyesha amepata kura 26,539 akitumia tiketi ya kujitegemea.

Mwaniaji wa Jubilee, Ashraf Hassan Awadh Bayusuf aliingia katika ukumbi wa ujumlishaji kupata haki yake ya asilimia 16.

Katika kampeni zake, Ali alikuwa akishikilia kuwa “kwa miaka 10 mfululizo nimekuwa nikisimama nanyi kuzidisha sauti zenu za kuhangaishwa. Sasa ni wakati wangu wa kuwauliza msimame nami katika harakati zangu za kuwania ubunge wa Nyali.”

Ameapa kuwa ushindi kibindoni, sasa atakuwa mshirikishi mkuu wa utawala wa haki kwa Wakenya wote bila ubaguzi. “Ingawa utawala wa haki na kimaadili umeonekana wazi kuhepa waheshimiwa bungeni, tusaidiane mimi niirejeshe haki hiyo ndani ya bunge letu,” akasema.

Huku hadi sasa akiwa amesalia katika orodha ya waajiriwa wa KTN katika mtandao wao rasmi akionekana kuwa bado ni mhariri wa upekuzi, ni kupotosha kwa hali ya sasa ambapo kwa sasa ni mheshimiwa mtarajiwa kwa kiapo cha huduma.

Chanzo: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako