If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Saturday, August 12, 2017

NASA: Tutakubali matokeo ya uchaguzi kwa masharti

Muungano wa upinzani wa NASA nchini Kenya umetangaza kuwa utakubali matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika juzi kote nchini humo iwapo utaruhusiwa kutazama data za asili katika sava za kumputa za Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya nchi hiyo (IEBC).

Hatua hiyo inatathminiwa kuwa, ni ishara ya kulegeza msimamo wa muungano wa upinzani ambao umekataa matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa na tume ya IEBC na kutoa wito wa kutangazwa mgombea wake, Bwana Raila Odinga kuwa ndiye mshindi wa uchaguzi wa Rais.

Wakala wa uchaguzi wa muungano wa NASA, James Orengo amewaambia waandishi habari mjini Nairobi kwamba, chama hicho kiko tayari kukubali matokeo ya uchaguzi iwapo IEBC itafungua sava za komputa za matokeo ya uchaguzi na kuruhusu NASA kutazama yaliyomo.

Awali Bwana Musalia Mudavadi ambaye ni Wakala Mkuu wa NASA katika uchaguzi huo amesema, vyanzo vyao vya siri ndani ya IEBC vimewapa ithibati kuwa Odinga amepata kura zaidi ya milioni nane huku Rais Uhuru Kenyatta aliyewania kiti hicho kwa muhula wa pili kupitia Chama cha Jubilee akipata kura milioni saba na laki saba.

Kuna hofu ya kutokea ghasia nchini Kenya

Msimamo wa sasa wa NASA uliotangazwa na James Orengo unatambuliwa kuwa ni aina fulani ya kulegeza kamba katika misimamo ya awali ya muungano huo.


Murithi Mutiga ambaye ni mwanachama wa kundi la International Crisis Group amesema msimamo wa sasa wa NASA ni dalili na kulegeza msimamo.

Hadi tunaingia mitamboni Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya ilikuwa ikisubiriwa kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu wakati wowote. Polisi na askari usalama wamesambazwa katika maeneo yote muhimu ya jiji la Nairobi kwa ajili ya kulinda usalama.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako