If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Saturday, August 12, 2017

UHURUTO TANO TENA

Na SAMMY WAWERU

RAIS Uhuru Kenyatta wa mrengo wa Jubilee na Naibu wake William Ruto wataongoza tena Jamhuri ya Kenya kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Uhuru Kenyatta
Uhuru Kenyatta wa Jubilee (kushoto). Kulia ni Raila Odinga wa muungano wa National Super Alliance (Nasa). Picha/MAKTABA

Matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika mnamo Jumanne Agosti 8, 2017 yametangazwa rasmi na mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC Bw Wafula Chebukati katika ukumbi wa Bomas.

Hii ni baada ya Kenyatta kuzoa kura 8,203,290 na kinara wa muungano wa National Super Alliance (Nasa) Raila Odinga kupata kura 6,762,224. Kenyatta amepata asilimia 54.27 huku Raila akipata asilimia 44.74 ya kura zilizopigwa.

Kulikuwa na jumla ya wapiga kura 19,687,563 waliosajiliwa na IEBC.

"Ninachukua fursa hii kumtangaza mheshimiwa Uhuru Kenyatta kuwa Rais wa tano wa Jamhuri ya Kenya akisaidiwa na mgombea mwenza William Ruto kama Naibu Rais," amesema Bw Chebukati mnamo Ijumaa saa nne na nusu za usiku baada ya kutangaza matokeo hayo rasmi katika ukumbi wa Bomas of Kenya.

Rais mteule; Kenyatta ameomba Wakenya wadumishe amani na kushirikiana na serikali yake kukuza taifa hili.

"Kenya itasalia kuwa moja. Tukashifu ghasia na ukabila. Tudumishe amani na tuishi kama jirani wema, ndugu na dada," amesema Rais Kenyatta baada ya kutangazwa mshindi kisha kupokezwa cheti cha kuchaguliwa akiandamana na Naibu wake Ruto, mkewe Bi Margaret Kenyetta, Bi Rachael Ruto mkewe Ruto.


Muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi, amefululiza hadi katika ukumbi wa KICC ambapo amehutubia taifa na kumshauri kinara wa Nasa Raila kwamba uchaguzi huo ulikuwa mashindano tu bali haufai kuleta chuki.

"Ndugu yangu mkubwa Raila Odinga, hayo yalikuwa mashindano tu kama kinyang'anyiro kingine, hayafai kuleta chuki kati yetu," amesema.

Kiongozi huyu aidha amesema atahudumia kila Mkenya pasi ubaguzi.

"Serikali yetu itahudumia watu wote milioni 45 kwa usawa bila ubaguzi. Ni haki ya kila mwananchi kuhudumiwa na serikali," akaeleza.

Akaongeza: "Tufanye kazi pamoja kwa minajili ya kukuza taifa letu."

Hata hivyo mrengo wa Nasa umekuwa ukishikilia kwamba unapinga kuchaguliwa kwa Rais Kenyatta ukishikilia kuwa shughuli hiyo ilikumbwa na wizi wa kura.

Awali Seneta wa Siaya James Orengo na kinara mwenza katika Nasa Musalia Mudavadi hawatambui matokeo hayo na kwamba Raila ndiye mshindi wa uchaguzi huo.

Wanadai kuwa mitambo ya IEBC ilidukuliwa na kumsaidia Rais Kenyatta kuibuka mshindi.

Kufikia sasa baada ya tume ya IEBC kumtangaza Rais Kenyatta kuwa mshindi, Nasa haijaeleza maoni yake hata baada ya Bw Chebukati kueleza kwa kina kura kutoka katika kila kaunti zilivyopigwa kabla hajatangaza mshindi ni nani.

Licha ya kusema kuwa wanapinga matokeo hayo, walisema kuwa hawataelekea mahakamani kukata rufaa na haifahamiki iwapo watabadilisha mawazo yao na kutaka haki katika idara ya mahakama.
Kinara wa Nasa Raila (ODM) aliwania wadhifa huo na mgombea mwenza Kalonzo Musyoka (Wiper).

Sasa Rais Kenyatta ana siku 14 (wiki mbili) kutoka leo Ijumaa ili aapishwa.
Tangazo hilo aidha litachapishwa kwenye gazeti la serikali kwa mujibu wa Katiba ya Kenya.

Source: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako