If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Wednesday, September 20, 2017

Historia ya Marhuma Bi Mwalim Fatma KamusNa Mohamed Omar Al Sheikh Bubakar (Juda)

Mapema Siku ya Jumatatu Tarehe 11 Sep 2017 sawa na Mwezi 20 Dhul Hijja, majira ya Saa Saba (Adhuhuri), jukwa la wanazuoni wa Zanzibar lilipatwa na pigo kubwa. Kwa masikitiko makubwa tumepokea msiba wa Maalim Bi. Fatma Muhamad Kamus.

INNA LILLAHI WAINNA ILAYHI RAJIOUN

Kifo ni haki kwa kila kiumbe cha Mwenye Enzi Mungu, bali kuondokewa na mwanachuoni mmoja katika ulimwengu huu, kuliziba kwake pengo hilo ni msiba mkubwa.

Mwanachuoni huyo alijulikana maarufu kwa jina la Mwalimu Bi Fatma Kamus, jina ambalo linatokana na kizazi cha Al Marhum Sheikh Mohamed Kamus, ambae naye alikuwa mwanachuoni Zanzibar aliyekuwa akiishi Mtaa wa Mbuyuni Mjini Unguja. Ni Sheikh ambae alisoma na kusomesha Msikiti wa Mbuyuni, na alikuwa Imam wa Msikiti wa Mbuyuni ujulikanao kwa Jina la Masjid Bakashmar.

Sheikh Mohamed Kamus alikuwa mwanafunzi wa Sheikh Said Bin Mohamed Dahman Laamudi. Sheikh Said Dahman nae alisoma na kupata elimu kubwa kwa Al Imam Habib Ahmad Bin Abibakar Bin Sumeity.

Marhemu Sheikh Mohamed Kamus aliyefariki dunia mwezi pili Ramadhan, alijaaliwa kupata kizazi cha Watoto sita. Na miongoni mwao ni Marhuma Bi.Fatma Kamus na Sheikh Kamus Mohamed Kamus ambae alikuwa Imam wa Msikiti wa Mbuyuni.

Sheikh Kamus Mohamed Kamus aliishika nafasi hii kufuatia kufariki baba yake, na akendelea na jukumu hili adhimu mpaka kufariki kwake Mwezi 16 Ramadhan 1418.

Mbali na Uimamu, Sheikh Kamus alifuata nyayo za baba yake na kuendeleza Darasa na kudumisha taratibu zote alizoachiwa na Baba yake Marehemu Sheikh Muhamed Kamus.


Na leo hii Mwezi 20 Dhul Hijja, amefariki Mwanachuoni huyu wa kike ambaye umri wake unakisiwa kufikia miaka 82 . Maisha yake yote akiishi mtaa wa Mbuyuni, akisomesha Madrassa za Qur' an kwa watoto na pia akisomesha Darasa za Tafsiri ya Qur' an, Hadithi, Balagha, Sira na Vitabu Vyengine. Halkadhalika alifungua darasa maalumu la ukoshaji maiti kwa upande wa wanawake.

Kazi iliyokuwa ikimpatia rizki yake ya kila siku, pia ilikuwa ualimu, ambapo alisomesha somo la Dini ya Kiislamu katika skuli ya Kajificheni Zanzibar mwaka 1973 mpaka 1994. 

Bi Fatma Kamus Alikuwa Mcha Mungu na mtu Mwema aliyewaheshimu watu wote bila kujali umri au tofauti nyengine zozote zile. Alipenda sana kuwausia na kuwahamasisha wanawake juu ya umuhimu wa kutafuta elimu.

Marhuma alikuwa mtu mpole, mnyenyekevu wa hali ya juu kabisa na mwenye taqwa. Wakati wote mdomo wake ulikuwa ukimtaja Mola wake pamoja na kumswalia Mtume Muhammad صلى الله عليه وسلم .

Kwa unyenyekevu wake na kumwogopa Mungu, kwa miaka mingi alikuwa akilala chini sakafuni, na kila alipoulizwa kwa nini anafanya hivi ilhali anacho kitanda, jibu lake ni moja tu, nalo ni kumuogopa Mola wake na kusema kwamba '' Kitanda kitanipumbaza kwa usingizi mzito, nakhofia isije ikanitokea nisiamke usiku kuswali Swala za usiku na ikanipita Swala ya Alfajiri''.

Alikuwa mlezi wa nyumba yote tokea asili ya wazee wake, alikuwa haridhiki ikifika Alfajiri mpaka awaamshe watoto wote. Kwa wanaume anawashika mkono mpaka Msikitini na kwa wanawake anahakikisha wote wanaamka na kuswali ila kwa mwenye udhuru maalum.

Tumeona jinsi malezi katika nyumba ya Mwanachuoni huyu yalivyokuwa, na namna alivyokuwa akiishi maisha yake yote.

Kabla ya kufariki ilipotimu saa 5 aliomba maji atawadhishwe alifanyiwa hivyo kama alivyotaka na mauti yakamfikia wakati huo huo.

Malezi haya Matukufu wameyapata kwa muasisi nae si mwengine bali ni baba yao. In shaa Allah Molah سبحانه وتعالى avijaalie na vizazi vyao na vyetu vishikamane na vijifananize Akhalaki zao njema.
Msikiti wa Mbuyuni ulijulikana kama Senior University ya Afrika Mashariki ukiwacha Ukutani Mjini Unguja, Zanzibar.

Marehemu Bi Fatma Kamus ameacha watoto watatu, wawili wa kiume na mmoja wa kike pamoja na wajukuu kadhaa. Aidha ametangulia mbele ya haki akiwaacha nyuma ndugu yake mmoja wa kiume, na ndugu zake wawili wa kike ambao nao pia ni walimu wa Madrasa za Qur'an.

Mtume Muhammad صلى الله عليه وسلم anatwambia مَن أكرَمَ عالِمًا فَقَد أكرَمَني
"Mwenye kumtukuza mwanachuoni, basi amenitukuza mimi"

Na pia Mtume wetu Muhammad صلوات الله وسلامه عليه ametuusia kwa kusema:
اذْكُرُوا مَحَاسِنَ مَوْتَاكُمْ وَكُفُّوا عَنْ مَسَاوِيهِمْ
[Wasemeni Maiti zenu kwa mazuri yao na kama hakuna ni bora kunyamaza]

Hapana shaka yeyote nasi tunafuata agizo hilo kwa kumzungumza Mama kama huyu aliyejitolea umri na uhai wake wote kumtumikia الله سبحانه و تعالى ili apate radhi zake. Na tunamuomba الله عز وجل amridhie na kumuingiza katika Pepo yake bila hisabu wala Ghadhabu.

Tunakuomba يا الله يا كريم kwa rehma zako utupokelee maombi yetu يا رب العالمين .
Nimalizie kwa Kumuomba Allah amsahe, Amghifirilie na amuweke na Waja wake Wema.
Na sisi sote الله سبحانه و تعالى atupe Mwisho Mwema. Aturuzuku Shahada kabla ya Mauti Yaarabbi.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako