If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Sunday, October 22, 2017

Kupanuka wigo wa uwepo wa wanajeshi wa Marekani barani Afrika na athari zake

Kupanuka wigo wa uwepo wa wanajeshi wa Marekani barani Afrika na athari zake
Kuuliwa wanajeshi wanne wa Marekani nchini Niger kumezidi kutoa mguso juu ya suala la kuhalalishwa kuongezwa idadi ya wanajeshi wa Marekani barani humo.

Wanajeshi wanne wa Marekani waliuliwa wiki iliyopita wakati walipokuwa kwenye doria ya pamoja katika eneo moja kusini magharibi mwa Niger kutokana na kuweko hatari kubwa ya waasi na makundi kama mtandao wa al Qaida wa eneo la Maghreb barani Afrika (AQIM).

Gazeti maarufu la nchini UIfaransa la Le Monde linalochapishwa kwa lugha ya Kifaransa limeandika kuwa idadi ya wanajeshi wa Marekani walioko Afrika chini ya anuani ya "utoaji mafunzo na uratibu wa majeshi ya nchi za Kiafrika na kushiriki katika mapambano dhidi ya makundi ya kigaidi" imeongezeka mara tatu katika miaka mitano iliyopita. Hivi sasa kuna zaidi ya wanajeshi 1300 wa kikosi maalumu cha Marekani barani Afrika suala ambalo linaonyesha kuwa Afrika baada ya Mashariki ya Kati limekuwa eneo la pili la uingiliaji kati wa Marekani duniani.

Hata kama kuuawa wanajeshi hao wa Marekani wiki iliyopita huko Niger kumeakisiwa pakubwa na vyombo vya habari na suala hilo kutoa mguso juu ya kuendelea kuwepo wanajeshi wa Marekani khususan katika eneo la Sahel barani Afrika, lakini ni miaka kadhaa sasa ambapo viongozi wa Marekani wamekuwa wakilitazama kwa jicho maalumu bara la Afrika; kiasi kwamba mwaka 2007 Rais wa wakati huo wa Marekani George W.Bush aliagiza kuasisiwa Kamandi ya Kijeshi kwa jina la AFRICOM kwa lengo la kusimamia oparesheni za kijeshi za nchi hiyo barani Afrika.

Wanajeshi wa Marekani wakitoa mafunzo kwa wanajeshi wa Niger

Kutokana na kuenea hatari ya ugaidi na kuongezeka makundi ya kigaidi na wanamgambo katika eneo la Afrika katika miaka ya hivi karibuni kwa upande mmoja; na katika upande wa pili, kuwepo mahasimu wa Washington katika eneo hilo kama Russia na Uchina, kumewafanya viongozi wa Marekani watoe zingatio maalumu kwa Afrika na wakati huo huo wazidishe vikosi vya nchi hiyo katika kalibu ya oparesheni za mafunzo ya kijeshi na zile za usaidizi.


Jeff Potter, Mkuu wa Taasisi iitwayo "North African Risk Advisory Board" amesema kuhusiana na suala hilo kuwa kamandi ya jeshi la Marekani barani Afrika ina mamia ya wanajeshi ambao baadhi yao wanatoa mafunzo na kulisaidia jeshi la Niger na pia kutekeleza shughuli za kijasusi na za kiutambuzi.

Japokuwa ripoti iliyotolewa na Thomas Waldhauser mkuu wa oparesheni za kikosi maalumu cha wanajeshi wa Marekani barani Afrika (AFRICOM), nchi hiyo inaeleza kuwa wanajeshi wa nchi hiyo wametumwa katika nchi mbalimbali za bara la Afrika ikiwemo huko Chad, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Somalia, Ethiopia, Uganda, Sudan, Rwanda na Kenya, lakini Marekani imejikita zaidi kijeshi katika baadhi ya nchi kama Niger kutokana na nafasi ya kistratejia ya nchi hiyo. Niger iko katikati ya korido ya eneo la Sahara yaani kati ya eneo lenye machafuko huko kaskazini mwa Mali na kusini mwa Libya; ambapo wanamgambo wenye misimamo mikali na makundi ya kigaidi yenye mfungamano na mtandao wa al Qaida na Daesh yapo katika maeneo yote mawili. Kupatiwa mafunzo na ndege za kivita wanajeshi wa Niger mwaka uliopita wa 2016 ni moja ya masuala yaliyozidisha kuimarika uhusiano baina ya nchi hiyo na Marekani.

Wanamgambo wenye silaha katika eneo la Sahel barani Afrika

Kwa mtazamo wa Washington bara la Afrika ni mahali pazuri kwa ajili ya kujikita kisiasa, kiuchumi na kijeshi madola makubwa ili kufanikisha malengo yao ya kikoloni. Kwa msingi huo, Washington imeandaa mikakati ya kunufaika na utajiri wa maliasili na kuhodhi masoko ya uchumi wa bara hilo. Kuhusiana na suala hilo, kuimarishwa uhusiano wa pande mbili, wa pande kadhaa, kustawishwa uhusiano na ushirikiano wa kijeshi kati ya Marekani na nchi za Kiafrika kwa upande mmoja; na katika katika upande wa pili kushadidisha machafuko kwa kuchochea vitisho vya kigaidi, hitilafu na mizozo ya ndani katika nchi za Kiafrika, ni masuala yanayopewa kipaumbele na viongozi wa Washington.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako