If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Thursday, December 14, 2017

HAJI MWINYI NA WENZAKE WAWILI KUUKOSA MCHEZO WA ZANZIBAR VS UGANDA

Mlinzi wa kushoto Mwinyi Haji Ngwali ataukosa mchezo wa kesho wa Zanzibar wakiwavaa mabingwa watetezi Uganda.

Zanzibar Heroes watakipiga na Uganda katika mchezo wa nusu fainali ya pili kwenye mashindano ya Cecafa Senior Challenge Cup, mchezo utakaopigwa saa 9:00 za Alaasiri kwenye uwanja wa Moi uliopo Kisumu.

Mwinyi ataukosa mchezo huo mara baada ya kupigwa kadi mbili za njano katika michezo miwili mfululizo iliyopita ukiwepo waliotoka sare ya 0-0 na Kenya na ule waliofungwa 1-0 na Libya ambapo kanuni ya mashindano hayo mchezaji akipewa kadi mbili mfululizo za njano katika michezo miwili mfululizo atalazimika kuukosa mchezo unaofuata.

Nafasi ya Mwinyi kesho itazibwa na Adeyum Ahmed Seif ambae pia ni mzoefu katika Mashindano hayo ya Cecafa.

Mbali ya Mwinyi pia Zanzibar Heroes itawakosa huduma za nyota wake wengine akiwepo mfungaji wao Kassim Suleiman Khamis pamoja na kiungo Amour Suleiman “Pwina” ambao wote ni majeruhi.

“Mwinyi hatocheza ana kadi 2 za njano, lakini pia Kassim na Amour nao tutawakosa kutokana na majeruhi”. Alisema Kocha wa Zanzibar Heroes Hemed Suleiman (Morocco).

Lakini kwa upande wa timu ya Uganda kesho itawakosa nyota wake wawili muhimu akiwemo Mulema Isaack na Awany Tinoethy ambao wote walipewa kadi mbili za manjano katika michezo miwili mfululizo iliyopita.

"Ni mechi ngumu nawajua sana Zanzibar lakini na sisi tutawaonyesha kama tunataka kulitetea kombe letu". Alisema Moses Basena kocha mkuu wa Uganda.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako