If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Wednesday, December 13, 2017

UAMUZI WA MAHAKAMA YA JUU WAKOSOLEWA VIKALI

Na BENSON MATHEKA

MAHAKAMA ya Juu imekosolewa kwa kukubaliana na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), ilipotoa uamuzi wa kina wa kutupilia mbali kesi za kupinga marudio ya uchaguzi wa urais wa Oktoba 26.

 Mahakama ya Juu
Kutoka kushoto: Majaji wa Mahakama ya Juu Njoki Ndung'u, Smoking Wanjala, Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu, Jaji Mkuu David Maraga, Jackton Ojwang' na Isaac Lenaola. PICHA/RICHARD MUNGUTI


Baadhi ya mawakili walisema kwamba uamuzi huo ni pigo kwa utawala wa sheria na utafutaji wa haki katika uchaguzi.

Kwenye uamuzi wao, majaji sita wa Mahakama ya Juu wakiongozwa na Jaji Mkuu David Maraga walisema uchaguzi ulikuwa huru na wa haki licha kutofanyika katika maeneobunge 25.

Msomi na mwanaharakati Profesa Makau Mutua alifananisha majaji hao na waliokuwa chini ya utawala wa Kanu ambao walikuwa wakiagizwa na serikali.

“Niliposikiliza majaji wa Mahakama ya Juu ya Kenya, niliona majaji waliohudumu katika utawala wa Kanu miaka iliyopita,” alisema Bw Mutua kwenye ujumbe wa twitter.

Mhadhiri wa chuo kikuu cha Nairobi Herman Manyora alisema uamuzi huo uliacha Wakenya wakijiuliza maswali mengi.

“Unaweza kutumiwa siku zijazo katika njia ambayo itayumbisha haki wakati wa uchaguzi hasa sehemu moja ya nchi ikikataa kupiga kura,” alisema.

Majaji walisema IEBC haikuzuia au kunyima yeyote nafasi ya kupiga kura.

Kwenye sababu za kutupilia mbali kesi za kupinga uchaguzi huo na ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta, majaji hao walikubaliana na IEBC kwamba kiongozi wa NASA Raila Odinga hakufuata sheria kujiondoa kwenye uchaguzi huo. Walisema kwamba Bw Odinga angejiuzulu siku tatu baada ya uteuzi.


Walishikilia kuwa IEBC haikustahili kufanya uteuzi mpya wakisema wagombezi wote walioshiriki uchaguzi wa Agosti 8 walipaswa kushiriki.

“Tunapata kuwa mshtakiwa wa kwanza (IEBC) kulingana na sheria, mgombeaji anaweza kujiondoa kwenye uchaguzi siku tatu baada ya uteuzi kwa kujaza fomu inayohitajika kisheria,” walisema majaji hao.

Hata hivyo, majaji hao walisema Rais Odinga alikuwa na haki ya kujiondoa katika uchaguzi huo wakisema hakuna mtu ambaye anafaa kulazimishwa kushiriki uchaguzi kinyume na mapenzi yake.

“Kwa kuandika barua kwa mshtakiwa wa kwanza, inachukuliwa kuwa Bw Odinga alimfahamisha kujiondoa kwake kwenye uchaguzi huo,” walisema majaji hao.

Hata hivyo, walisema hatua hiyo haingefanya uchaguzi huo kufutiliwa mbali walivyodai walalamishi.

Kulingana na majaji barua ya Bw Odinga ilikuwa ilani ya kutaka kujiondoa kwenye uchaguzi. “Kuna utaratibu wa kujiondoa kwa kujaza fomu inayohitajika,” walisema.

Aidha, walikubaliana na uamuzi wa Jaji John Mativo wa Mahakama Kuu kwamba uamuzi wa Mahakama ya Juu katika kesi ya kupinga matokeo ya kura ya urais 2013 hauwezi kutumiwa kutilia nguvu kesi.

Walisema sehemu ya uamuzi huo ambayo walalamishi walitaja kama maoni ya majaji kujibu swali waliloulizwa na Mwanasheria Mkuu na hayawezi kutumiwa kama msingi wa kisheria.

Chanzo: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako