If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Wednesday, April 25, 2018

Polisi Tanzania yaimarisha usalama kuhusu maandamano, nayo Chadema yayakana

Polisi Tanzania yaimarisha usalama kuhusu maandamano, nayo Chadema yayakana
Jeshi la Polisi nchini Tanzania limeimarisha usalama kila kona ya nchi, kutokana na tetesi za kufanyika maandamano ya kesho tarehe 26 Aprili na ambayo yamekuwa yakihimizwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii kwa ajili ya kupinga serikali ya Rais John Pombe Magufuli wa nchi hiyo.

Kufuatia hali hiyo polisi imewataka wananchi wote kuendelea na shughuli zao kama kawaida kwa kuwa maandamano yanayozungumzwa hayapo na kwamba ni batili. Akizungumza leo jijini Dar es Salaam kaimu kamanda wa Polisi Kanda Maalum, ACP Sweethbert Njwele amesema jeshi la polisi limejipanga kuhakikisha kila mtu anafanya shughuli zake kama kawaida bila kuvunja amani hapo kesho.

Maandamano ya wapinzani nchini Tanzania

Hayo yanajiri katika hali ambayo, mapema jana serikali ya Uingereza iliwaonya raia wake wanaoishi Tanzania kuhusiana na maandamano hayo tarajiwa. "Niwahakikishie, jeshi la polisi tumejipanga hakuna maandamano yatakayofanyika hivyo kila mtu aendelee na shughuli zake kama kawaida." amesema Njwele. 

Akizaungumza na shirikisho la waendesha pikipiki maarufu kama 'bodaboda' jijini Dar es Salaam kwa upande wake msemaji wa shirikisho la waendesha pikipiki Adamu Kyando amesema: "Kuna taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikihamasisha bodaboda kushiriki maandamano taarifa hizi si za kweli na ni batili."

Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania


Hayo yanajiri katika hali ambayo Mwenyekiti wa Chadema, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja, Idrissa Jumbe Mkila, amesema chama hicho hakihusiki na maandamano yoyote yanayotarajiwa kufanyika kesho. 

Mkila ameyasema hayo leo Aprili 25 wakati akizungumza na waaandishi wa habari katika ufunguzi wa mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo viongozi wa chama Wilaya na Mikoa huko Kikwajuni Mkoa Mjini Unguja. 

Ni muda sasa ambapo kumekuwepo kauli kuhusiana na maandamano tarajiwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii chini Tanzania suala ambalo limelifanya jeshi la polisi nchini humo kuchukua tahadhari.

Chanzo: parstoday.com 

No comments:

Post a Comment

Maoni yako