If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Thursday, July 12, 2018

Ethiopia: Kufunguliwa tena barabara zinazoelekea katika bahari Nyekundu ni kipaumbele

Ethiopia: Kufunguliwa tena barabara zinazoelekea katika bahari Nyekundu ni kipaumbele
Ethiopia imesema kuwa inataka kulipa kipaumbele suala la kuzifungua tena barabara mbili zinazoiunganisha nchi hiyo na bandari mbili za Eritrea zilizopo katika bahari Nyekundu kufuatia kufikiwa mapatano baina ya nchi mbili hizo.

Nchi mbili hizo jirani za Pembe ya Afrika Jumatatu iliyopita zilikubaliana kufungua balozi zao, kuendeleza shughuli za bandari na kuanzisha tena safari za ndege kati ya pande mbili baada ya nchi mbili hizo kufikia mapatano yaliyohitimisha mzozo wa miaka 20 baina ya nchi hizo jirani. Weledi wa mambo wanasema kuwa mapatano hayo ya kihistoria huenda yakapelekea kutekelezwa mageuzi ya kisiasa na kiusalama katika eneo la Pembe ya Afrika lililokumbwa na maachafuko.

Ahmed Shide msemaji wa serikali ya Ethiopia amesema kuwa kufunguliwa tena kwa barabara hizo muhimu zinazoelekea katika bandari za Assab kusini mwa Eritrea na huko Massawa kaskazini mwa nchi hiyo kutakuwa kwa manufaa ya eneo zima.

Aidha jana Jumatano Waziri Mkuu wa Ethiopia Ahmad Abiy aliandika katika mtandao wake wa kijamii wa twitter kwamba raia wa Ethiopia na Eritrea wenye hati za kusafiria wanaweza kufanya safari katika nchi mbili hizo na kupewa viza baada ya kuwasili.

Ahmed Abiy, Waziri Mkuu wa Ethiopia

No comments:

Post a Comment

Maoni yako