If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Monday, October 15, 2018

MUNGATANA AELEZEA JINSI ALIVYOTAPELIWA NA WAJUAJI

Na LEONARD ONYANGO/ NAIROBI, Kenya

ALIYEKUWA mbunge wa Garsen Danson Mungatana hatimaye ameelezea masaibu yake baada ya kupoteza mamilioni ya fedha kwa walaghai.

Danson Mungatana
Danson Mungatana ahutubia wanahabari Oktoba 15, 2018, katika hoteli ya Laico Regency. Picha/EVANS HABIL

Bw Mungatana, hata hivyo, Jumatatu amekanusha madai kwamba alihadaiwa na waganga waliomwahidi kumzalishia fedha awe bilionea.

Mbunge huyo wa zamani aliyekuwa akihutubia wanahabari jijini Nairobi amesema alikuwa mwathiriwa wa utapeli uliohusisha wafanyabiashara mashuhuri wa humu nchini na raia wa kigeni.

Amesema matapeli hao walianzisha mradi wa uwekezaji uliohusisha ununuaji na uuzaji wa mafuta.

Matapeli hao waliwataka mabwanyenye wa humu nchi kuwekeza katika mradi huo kwa kuwapa ahadi kwamba wangelipwa kiasi kikubwa cha faida.

“Mara ya kwanza tulipewa mgawo wa faida, mara ya pili pia tukapewa mgawo huo. Mara ya tatu raia hao wa kigeni walitoweka na fedha zetu,” akasema Bw Mungatana ambaye pia amewahi kuwa waziri msaidizi wa Huduma za Matibabu.

Kulingana na ripoti zilizochapishwa katika baadhi ya vyombo vya habari, Bw Mungatana alitapeliwa Sh76 milioni.

Mamilioni yapotea


Hata hivyo yeye amekataa kufichua kiasi cha fedha alizopoteza na badala yake akasema kuwa “nilipoteza mamilioni ya fedha.”

Raia wa kigeni waliotambuliwa kwa majina ya Abdoulaye Tamba, Abdalla Tamba – wote raia wa Chad pamoja na Anthony Mwangangi ambaye ni dereva wao tayari wanazuiliwa rumande baada ya mahakama kuagiza wazuiliwe kwa siku 15 kuwezesha polisi kukamilisha uchunguzi wao.

Washukiwa hao walinaswa na maafisa wa upelelezi katika eneo la Brookside Drive mtaani Westlands, Nairobi ambapo walipatikana noti ghushi Sh1 bilioni.

“Polisi walinasa washukiwa mnamo Septemba 28 na wakawataka Wakenya ambao wametapeliwa kujitokeza na kuwatambua washukiwa hao. Nilimtambua Abdalla Tamba ambaye ni mmoja wa watu walionitapeli kwa njia tofauti sana na uchawi kama ilivyodaiwa,” akasema Bw Mungatana.

“Sikutaka kuwa bilionea kwa siku moja namna inavyodaiwa. Mama yangu hakunifundisha kutafuta utajiri wa haraka kwa kutumia njia za mkato. Nimekuwa mchapakazi tangu nilipozaliwa,” akaongezea.

Wakili huyo alishutumu baadhi ya vyombo habari kwa ‘kunifanya kuonekana mjinga baada ya kutapeliwa’.

“Ni kweli nilisomea katika shule ya Upili ya Alliance na nikafanya vyema katika Chuo Kikuu cha Nairobi. Kwa sasa nasomea Uzamifu (PhD). Naona kwamba uhalifu huo unaweza kutokea kwa yeyote. Uhalifu hauheshimu digrii au masomo,” akasema.

Kulingana na Bw Mungatana watu mbalimbali maarufu walinaswa na mtego wa matapeli hao lakini hawajaripoti kwa sababu wanaogopa kukejeliwa.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako