If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Tuesday, August 28, 2018

NAIROBI: MOMBASA EXPRESSWAY KUJENGWA NA BECHTEL CORPORATION

Na SAMMY WAWERU na MASHIRIKA, WASHINGTON D.C./ NAIROBI

SERIKALI ya Marekani na ya Kenya imekubaliana kutengeza barabara ya njia nne, sawa na Thika Superhighway itakayounganisha mji wa Mombasa na jiji kuu la Nairobi.

Donald Trump
Rais Donald Trump wa Marekani akimsalimia Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya katika ofisi ya kiongozi huyo wa Marekani, White House Agosti 27, 2018, jijini Washington, D.C. Picha/AFP

Hii ni baada ya Rais Uhuru Kenyatta na Rais Donald Trump wa Marekani kukutana mnamo Jumatatu katika Ikulu ya White House, Washingon D.C.

Taarifa kutoka Ikulu hiyo iliyotumwa kwa vyombo vya habari mapema Jumanne, inasema viongozi hao waliafikiana kuunda barabara hiyo itakayojulikana kama 'Nairobi-Mombasa Expressway'.

Barabara hiyo itajengwa na kampuni kubwa ya uhandisi, Bechtel Corporation ya Marekani.

Rais Trump na Kenyatta walifanya kikao cha faragha katika ofisi ya Trump, Oval ambapo walijadili mikakati ya kuimarisha uhusiano kati ya Kenya na Marekani.Ili kufanikisha uundaji wa barabara hiyo, Kenya na Marekani imekubaliana kufanya mashauriano zaidi ya kufadhili mradi huo. "Pande zote mbili zimekubaliana kufanya mashauriano ili kuweka mikakati ya kufadhili mradi wa barabara hiyo," shirika la habari la Agence France Presse, lenye makao yake makuu jijini Paris Ufaransa lanukuu taarifa hiyo.

Mchambuzi wa masuala ya kisiasa Kenya na mwenye uelewa kuhusu masuala muhimu ya kijamii ameliambia shirika moja la kimataifa kwamba hii ni njama ya Marekani kunyonya Kenya.


"Ninahisi Marekani inajitafutia biashara kubishana na China ambayo imepanua mawanda yake katika ushirikiano na mataifa ya Bara la Afrika," amesema mchambuzi Herbert Manyora.

Thika Superhighway inayounganisha mji wa Thika na jiji la Nairobi, iliundwa chini ya serikali ya mseto iliyoongozwa na Rais (mstaafu) Mwai Kibaki na kiongozi wa Orange Democratic Movement (ODM) Raila Odinga, akiwa Waziri Mkuu.

Mradi huo uligharimu Sh27 bilioni, na barabara hiyo ina umbali wa kilomita 50. Kati ya Mombasa na Nairobi, kuna umbali wa kilomita 441.

Rais Kenyatta na Trump, pia walijadili jinsi ya kuimarisha sekta ya utalii, biashara, amani na usalama, na miundo msingi mingine ya kuimarisha uchumi wa mataifa haya mawili ili kuwafaa raia wake.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako