If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Friday, August 17, 2018

Seneti ya Marekani yapasisha azimio dhidi ya sera za kidikteta za Trump

Seneti ya Marekani yapasisha azimio dhidi ya sera za kidikteta za Trump
Baraza la Seneti la Marekani limepasisha azimio linalokosoa mienendo ya rais wa nchi hiyo dhidi ya vyombo vya habari.

Azimio hilo lililopasishwa na Baraza la Seneti la Marekani limemkosoa Rais Donald Trump kutokana na tabia yake ya kuvituhumu vyombo vya habari kuwa ni "adui wa wananchi".

Azimio hilo limepasishwa baada ya zaidi ya magazeti 300 ya Marekani kuchukua hatua ya pamoja ya kutetea uhuru wa vyombo vya habari na kumkosoa Donald Trump kutokana na kushambulia kwake baadhi ya vyombo vya habari vinavyohoji na kukosoa sera zake za ndani nje ya nchi.

Magazeti zaidi ya 350 kote nchini Marekani jana Alkhamisi yalijibu tuhuma za Trump aliyeviita vyombo vya habari kuwa ni "adui wa wananchi" kwa kutenga tahariri zao kwa ajili ya makala za kutetea uhuru wa vyombo vya habari.

Rais Donald Trump wa Marekani amekuwa akishambulia waandishi habari na ripoti zinazotofautiana na kupinga misimamo yake ya kisiasa na kuzitaja habari na ripoti zao kuwa ni bandia.

Vilevile ofisi za gazeti la The Boston Globe ambalo ndilo lililobuni fikra ya kuyashirikisha magazeti zaidi ya 350 ya Marekani katika kampeni hiyo ya kutetea uhuru wa vyombo vya habari dhidi ya sera za kidikteta za Trump, zimetishiwa kulipuliwa kwa mabomu.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako