If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Friday, September 7, 2018

Kijana mwenye silaha ashambulia benki nchini Marekani, watu kadhaa wuawa

Kijana mwenye silaha ashambulia benki nchini Marekani, watu kadhaa wuawa
Kwa akali watu 4 wameuawa na wengine 4 kujeruhiwa wakiwa katika jengo la benki katika mji wa Cincinnati wa jimbo la Ohio nchini Marekani baada ya kushambuliwa na kijana aliyekuwa na silaha.

Duru za habari zimearifu kwamba kijana huyo aliyekuwa na silaha aliingia katika jengo la benki la mji huo na kuanza kumiminia risasi ambapo watu wanne waliuawa na wengine wanne kujeruhiwa. Polisi ya mji wa Cincinnati mbali na kufunga maeneo jirani na benki hiyo imetangaza kwamba, mshambuliaji aliuawa katika tukio hilo. Hata hivyo haijulikani iwapo kijana huyo alijipiga risasi mwenyewe au aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi.

Hadi sasa bado hakujatolewa taarifa kamili za kijana aliyefanya shambulizi hilo.

Kijana aliyefanya shambulizi hilo

Marekani imekuwa ikikumbwa na wimbi la vitendo vya utumiaji mabavu, utekaji nyara na mashambulizi ya watu wenye silaha. Kwa mwaka maelfu ya watu huuawa kwa kupigwa risasi katika maeneo tofauti ya nchi hiyo inayojinadi kuwa polisi ya dunia. Kwa mujibu wa ripoti rasmi, karibu silaha za moto milioni 270 hadi 300 zinamilikiwa na raia, hii ikiwa na maana kwamba, karibu kila raia mmoja wa Marekani anamiliki silaha ya moto. 

Licha ya makundi ya kutetea haki za binaadamu nchini Marekani ktoa wito wa kuwekwa sheria kali ya kuzuia uuzaji silaha za moto nchini humo, lobi za magenge yanayouza silaha zimezuia kuchukuliwa hatua yoyote katika uwanja huo. Vilevile Rais Donald Trump wa Marekani ni miongoni mwa waungaji mkono wakuu wa umiliki silaha.

Eneo lililoshambuliwa

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako