If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Thursday, September 13, 2018

RAIS KENYATTA AFANYA MABADILIKO MAKUBWA IDARA YA POLISI

Na SAMMY WAWERU, LOWER KABETE, Kenya

RAIS Uhuru Kenyatta amezindua mfumo mpya wa utendakazi katika idara ya polisi (NPS) anaoamini utaleta mabadiliko makuu na kwamba unaleta taswira mpya katika idara hiyo.

Rais Uhuru Kenyatta
Rais Uhuru Kenyatta akihutubia taifa awali. Picha/MAKTABA

Akihutubu Alhamisi katika kongamano la maafisa wa polisi nchini lililofanyika katika Taasisi ya Mafunzo ya Kiserikali (KSG) iliyoko Lower Kabete, Nairobi alisema mabadiliko hayo yanalenga kufanya idara hiyo kuwa ya kuaminika na kuheshimika.

"Yanapania kuimarisha utendakazi wa maafisa wetu uwe bora, kutoka ule wa amri hadi huduma kwa taifa," amesema Rais Kenyatta.

Kwenye mfumo huo mpya, Naibu Inspekta Mkuu (IG) kutoka kwa polisi wa kawaida amepewa majukumu ya kuangazia usalama wa umma nchini.

Kiongozi huyo wa taifa ameeleza kuwa litakuwa jukumu la afisa huyo kuhakikisha kila Mkenya yuko salama, huku Naibu Inspekta Mkuu (IG) kutoka kitengo cha askari tawala (AP) akikabidhiwa majukumu ya kuhakikisha boda za Kenya ziko salama.

Kitengo cha upelelezi wa jinai, kilicho chini ya mkurugenzi mkuu wake (DCI) George Kinoti, pia kimepata mabadiliko ya majukumu ambapo kitahitajika kuhakikisha uchunguzi wa visa vya uhalifu umefanyika kwa kina na uwazi.

AP na maafisa wa polisi wa kawaida


Polisi tawala na wale wa kawaida wamechanganywa ambapo watakuwa wakifanya majukumu pamoja.

AP wameruhusiwa kukamata na kufungulia mshtakiwa mashtaka kortini.

"Nyinyi watu wa magazeti msiende kuandika tumeondoa utawala wa AP. Maafisa hao sasa wana nguvu kukamata na kufunga, iwapo ulidhani AP hawana wajibu huo sasa jua wazi kuwa atakukamata na kukufikisha kortini," akafafanua Kenyatta. Awali, maafisa wa kawaida ndio pekee waliruhusiwa kukamata mshukiwa wa uhalifu na kumfikisha kortini.

Kiongozi huyo wa taifa pia amezindua sare mpya kwa idara ya polisi, ikiwa ni pamoja na kubadilisha majina ya vyuo vya mafunzo kwa makrutu. Miongoni mwa ajenda kuu za Rais Kenyatta, ni kuwepo kwa makazi bora kwa kila Mkenya, na ametangaza kuondoa makazi ya maafisa wa polisi ambapo ameamuru kila afisa apewe marupurupu ya nyumba.

Kwa muda mrefu maafisa wa polisi wamekuwa wakiishi kwa makazi duni, na Rais amesema marupurupu hayo yatawawezesha kukodi nyumba bora.

Waziri wa Usalama wa Ndani Dkt Fred Matiang'i ndiye amekabidhiwa wajibu huo kuhakikisha mabadiliko hayo yamefanyika.

Wizara ya Fedha na Hazina ya Kitaifa, imeagizwa kutoa pesa mara moja zitakazotumika kufanya mabadiliko hayo, miongoni mwa mengine katika idara hiyo. Henry Rotich, ndiye Waziri wa Fedha.

Rais Kenyatta alikabidhiwa ripoti ya mabadiliko hayo na Dkt Matiang'i ili kuyatanagaza rasmi kwa taifa. Matiang'i alisema wizara yake inafanya kazi kwa karibu na kushauriana na washikadau husika kuhakikisha idara ya usalama imeimarika.

"Tunataka idara ya polisi inayotusongesha mbele. Tunashauriana na washikadau husika kama vile ya habari na mawasiliano (ICT) ili kufanikisha utendakazi bora wa idara ya usalama," akasema waziri huyo.

Inspekta Mkuu wa Polisi (IG) Joseph Boinnet, alisema idara yake iko ange kufanya kazi kikamilifu. Alisema mabadiliko katika idara hiyo yanasaidia kuimarisha utendakazi wa maafisa wake.

Waliohudhuria uzinduzi wa mfumo huo ni; waziri wa habari na mawasiliano (ICT) Joe Mucheru, Najib Balala (Utalii), Faridah Karoney (Ardhi), Profesa Margaret Kobia (Utumishi wa Umma, Vijana na Jinsia), mwenyekiti wa idara ya polisi (NPS) Johnstonne Kavuludi, makatibu wa wizara mbalimbali, miongoni mwa viongozi wengine wakuu serikalini.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako