If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Sunday, September 2, 2018

Uchaguzi wa bunge waanza Rwanda, RPF yatabiriwa ushindi

Uchaguzi wa bunge waanza Rwanda, RPF yatabiriwa ushindi
Wananchi wa Rwanda wameanza kupiga kura katika uchaguzi wa bunge ambao unatazamiwa kukipa ushindi chama tawala cha Rwanda Patriotic Front (RPF).

Upigaji kura ambao umeanza leo Jumapili unatazamiwa kuendelea kwa siku tatu katika vituo 2,500 vya upigaji kura katika nchi hiyo ndogo ya Afrika Mashariki.

Kuna watu zaidi ya milioni saba waliojiandikisha kupiga kura kuwachagua wajumbe katika bunge lenye viti 80 ambapo, viti 24 ni maalumu kwa wanawake, viwili ni vya vijana na kimoja cha walemavu.

Wagombea zaidi ya 500 kutoka vyama vitano vya kisiasa na wagombea wanne huru wanashiriki katika uchaguzi huo.

Weledi wa mambo wanatazamia kuwa chama cha RPF cha Rais Paul Kagame kitadumisha wingi wake wa viti bungeni ambapo sasa kina viti 76.

Rais Paul Kagame akipiga kura

Walemavu na Wanyarwanda wanaoishi nje ya nchi wanapiga kura leo na kesho wabunge 53 watapigiwa kura. Siku ya Jumanne wapiga kura watawachagua wabunge 24 wa kike na wawakilishi wawili wa vijana.

Matokeo ya uchaguzi yamepangwa kutangawa Septemba 16.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako