If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Thursday, September 13, 2018

Umoja wa Mataifa walaani kukandamizwa wanaharakati wa haki za binadamu katika nchi 38 duniani

Umoja wa Mataifa walaani kukandamizwa wanaharakati wa haki za binadamu katika nchi 38 duniani
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani vitendo vya ulipizaji kisasi na vitisho dhidi ya wanaharakati wa masuala ya kutetea haki za binadamu katika nchi 38 duniani na kuvitaja kuwa ni fedheha kubwa.

Antonio Guterres amesema hayo katika ripoti yake maalumu ambapo amezitaja nchi 38 duniani ikiwemo Saudi Arabia na Bahrain kwamba, zimekuwa zikifanya ukandamizaji dhidi ya wanaharakati wa haki za binadamu.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema katika ripoti yake hiyo kwamba, nchi hizo 38 zimekiuka haki za binadamu kwa kufanya mauaji, mateso na kukamata watu kiholela lengo likiwa ni kulipiza kisasi au kuwatisha wanaharakati wa haki za binadamu.

Aidha jinai za utawala haramu wa Israel dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina zimetajwa katika ripoti hiyo ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwamba, ni ukiukaji wa wazi wa haki za binadamu.

Saudi Arabia ni miongoni mwa nchi zinazokiuka haki za binadamu duniani

Ripoti ya Antonio Guterres imejumuisha pia masuala kama miamala mibaya, ujasusi, kupandikizia watu kesi na kampeni ya kuwachafulia majina wanaharakati wa haki za binadamu.


Kadhalika imekuja katika ripoti hiyo ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwamba, serikali husika zimekuwa zikiwatuhumu wanaharakati wa haki za binadamu kwamba, wanafanya ugaidi na kushirikiana na mamluki wa kigeni au kufanya njama za kuvuruga usalama wa nchi.

Tawala kandamizi za Mashariki ya Kati kama Bahrain, Saudi Arabia na Israel ambazo zimekuwa zikikiuka wazi haki za binadamu daima zimekuwa zikiungwa mkono na Marekani na madola ya Magharibi yanayodai kuwa watetezi wa haki za binadamu.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako