If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Thursday, October 4, 2018

Naibu Waziri wa zamani wa US: Serikali ya Trump haitaki mkataba wowote wa kimataifa

Naibu Waziri wa zamani wa US: Serikali ya Trump haitaki mkataba wowote wa kimataifa
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani wa Marekani Wendy Sherman amekosoa hatua ya serikali ya nchi hiyo ya kujitoa kwenye Mkataba wa Uhusiano Mwema wa mwaka 1955 iliyosaini baina yake na Iran na kueleza kwamba si kitu cha ajabu kwa serikali isiyopenda kuheshimu makubaliano yoyote ya kimataifa kuchukua hatua hiyo.

Bi Sherman, ambaye alikuwa mjumbe mwandamizi wa ujumbe wa Marekani katika mazungumzo ya nyuklia ya Iran na kundi la 5+1 amesema, Donald Trump na mshauri wake wa usalama wa taifa, John Bolton hawapendi mkataba wowote ule wa kimataifa.

Ameongeza kuwa: Imani aliyonayo Trump ni juu ya mielekeo ya utaifa na misimamo ya kujitawala kiutaifa tu, wala hapendi kuwepo ushirikiano wa baina ya pande kadhaa duniani.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani wa Marekani amebainisha kuwa serikali ya Trump inaitumia fursa iliyonayo hivi sasa kwa ajili ya kukoleza moto tu wa hatua zake dhidi ya Iran.

Baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu (ICJ) kutoa hukumu hapo jana kwa manufaa ya Iran kufuatia mashtaka iliyofungua Tehran kwenye mahakama hiyo ya kuishtaki Marekani, serikali ya Washington ilitangaza jana hiyohiyo kwamba inajitoa kwenye Mkataba wa Uhusiano Mwema iliosaini na Iran mwaka 1955.

Rais Donald Trump wa Marekani (kushoto) na John Bolton, mshauri wake wa usalama wa taifa

Lakini sambamba na uamuzi huo, mshauri wa usalama wa taifa wa Marekani John Bolton alitangaza hapo jana pia kwamba, kwa amri ya rais wa nchi hiyo Donald Trump, Washington inajitoa pia kwenye Mkataba wa Hiyari wa Vienna wa mwaka 1961. 


Hii ni kufuatia hatua iliyochukuliwa siku ya Jumamosi iliyopita na Palestina ya kufungua mashtaka kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu kupinga hatua ya Washington ya kuhamishia ubalozi wake katika mji wa Baitul Muqaddas ambao ni mji mkuu wa Palestina.

Kwa mujibu wa mkataba wa Vienna, kila nchi inatakiwa iweke ubalozi wake katika ardhi ya nchi mwenyeji; katika hali ambayo utawala wa Kizayuni wa Israel unaukalia kwa mabavu mji wa Baitul Muqaddas baada ya kuuvamia kijeshi na kudai tu kwamba una mamlaka nao ya kiutawala. Kwa sababu hiyo Marekani inalazimika kuwaondoa wanadiplomasia wake katika mji huo.../

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako