If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Monday, October 15, 2018

Raia wanne wauawa katika maeneo yanayozungumza Kiingereza nchini Cameroon

Raia wanne wauawa katika maeneo yanayozungumza Kiingereza nchini Cameroon
Mratibu wa jumuiya ya kutetea haki za binadamu nchini Cameroon ametangaza habari ya kuuawa watu wanne katika mji wa Mutengene wa kusini magharibi mwa nchi hiyo.

Aziz Moustapha ametangaza habari hiyo na kuongeza kuwa watu hao wanne wameuawa baada ya jeshi la Cameroon kushambulia nyumba zao katika eneo lenye wazungumzaji wengi wa Kiingereza la kusini magharibi mwa nchi hiyo.

Maximilienne Ngo Mbe, mkurugenzi mtendaji wa kanali ya kutetea haki za binadamu katika eneo la katikati mwa Afrika naye amesema katika mkutano uliofanyika Yaoundé, mji mkuu wa Cameroon kuwa, tangu miezi kadhaa nyuma kumewekwa amri ya kutotoka nje katika maeneo yenye wazungumzaji wengi wa Kiingereza nchini humo na jeshi la Cameroon linaingia katika nyumba moja baada ya nyingine kuua watu ambao hawana vitambulisho.

Eneo la kusini magharibi mwa linalopigania kujitenga na Cameroon

Machafuko yameongezeka sana kwenye miezi ya hivi karibuni katika maeneo yenye wazungumzaji wengi wa Kiingereza nchini Cameroon.

Wazungumzaji wa Kiingereza wanaunda karibu asilimia 20 ya wakazi wote milioni 20 wa Cameroon. Wazungumzaji hao wa Kiingereza wanalalamika kuwa wananyanyaswa na kutengwa na serikali kuu na wananyimwa haki zao kama raia wa Cameroon hivyo wanaona ni vyema wapiganie kujitenga.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako