If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Monday, October 22, 2018

Uingereza, Ujerumani na Ufaransa zatoa taarifa ya pamoja kulaani mauaji ya Khashoggi

Uingereza, Ujerumani na Ufaransa zatoa taarifa ya pamoja kulaani mauaji ya Khashoggi
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, Ujerumani na Ufaransa wametoa taarifa ya pamoja na kulaani kuuliwa mwandishi habari mkosoaji wa utawala wa Saudi Arabia.

Jean-Yves Le Drian Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Jeremy Hunt Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza na Heiko Maas wa Ujerumani wametangaza katika taarifa yao hiyo kuwa hakuna jambo linaloweza kuhalalisha mauaji ya Jamal Khashoggi mwandishi habari aliyekuwa akiukosoa utawala wa Saudi Arabia.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa kutolewa vitisho, kushambuliwa na kuuliwa waandishi wa habari ni jambo lilisokubalika kwa hali yoyote ile na kwamba masuala hayo yanazitia wasiwasi mkubwa nchi tatu za Ulaya yaani Ujerumani, Ufaransa na Uingereza. Mawaziri hao wa Mambo ya Nje wa nchi tatu za Ulaya wamepinga kitendo cha Saudi Arabia cha kuhalalisha namna Khashoggi alivyouliwa na kusisitiza kuwa kunahitajika kuwekwa wazi haraka iwezekanavyo kuhusu kile kilichojiri. Jamal Khashoggi mwandishi habari mkosoaji wa utawala wa Saudi Arabia alitoweka baada ya kuingia katika ubalozi mdogo wa Saudia mjini Istanbul Uturuki tarehe pili mwezi huu na siku kadhaa zilizofuata vyombo vya habari viliripoti kuhusu kuuawa kwake. Hatimaye siku ya Jumamosi tarehe 18 mwezi huu utawala wa Saudia ulithibitisha kuwa Jamal Khashoggi aliuliwa ndani ya ubalozi wake huo mdogo huko Istanbul hata hivyo ukadai kuwa aliaga dunia baada ya kutokea mapigano baina yake na mtu mmoja.

Jamal Khashoggi, mwandishi habari aliyeuliwa katika ubalozi mdogo wa Saudi Arabia nchini Uturuki

Viongozi wengi wa dunia akiwemo Bi Angela Merkel Kansela wa Ujerumani ameyataja madai hayo ya Riyadh kuwa simulizi za uwongo.

Chanzo: http://parstoday.com/

No comments:

Post a Comment

Maoni yako