If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Tuesday, October 16, 2018

Wacomoro waandamana kupinga jaribio la Rais wa nchi hiyo la kurefusha utawala wake

Wacomoro waandamana kupinga jaribio la Rais wa nchi hiyo la kurefusha utawala wake
Wananchi wa Comoro jana walifanya maandamano na kufunga barabara za mji wa Anjouan wakipinga jitihada zinazofanywa na Rais Azali Assoumani wa nchi hiyo za kutaka kurefusha kipindi cha uongozi wake na kukomesha mfumo wa kuongoza kwa zamu baina ya visiwa vitatu vikuu vinavyounda Jamhuri ya watu wa Comoro.

Mabadiliko hayo ambayo yatamuwezesha Azali Assoumani kugombea tena kiti cha rais wa Comoro mwaka 2019 yamewakasirisha wakazi wa kisiwa cha Anjouan kwa sababu yatawanyima haki ya kuwa na rais katika mfumo wa wasa wa kuongoza nchi kwa zamu baina ya visiwa vitatu vya Jamhuri ya Comoro.

Waandamanaji kisiwani Anjouan walikabiliana kwa mawe na askari waliojaribu kutuliza maandamano hayo.

Afisa wa serikali katika kisiwa hicho, Mohamed Sadate Nadjib amesema maandamano hayo ni matokeo ya kuchoshwa na maamuzi mabaya yaliyochukuliwa na Rais Azali.

Mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu kiongozi wa Comoro aliitisha kura ya maoni ya kurefusha kipindi cha uongozi wa rais ambayo inamruhusu Azali Assoumani kugombea tena kwa vipindi vingine viwili vya miaka mitano mitano kuanzia uchaguzi uliopangwa kufanyika mapema mwakani.

Azali Assoumani


Kambi ya upinzani nchini Comoro ilipinga zoezi hilo la kura ya maoni lililofanyika tarehe 30 Juni na kumtuhumu Rais Asoumani kuwa amekiuka katiba.

Katiba ya sasa ya Comoro inaamuru kuwa nafasi ya rais inapaswa kuchukuliwa kwa zamu na kwa kupokezana baina ya viongozi wa visiwa vitatu vikuu vya nchi hiyo ambavyo ni Ngazidja Mohéli na Anjouan.

Azali Assoumani anajiunga na viongozi kadhaa wa nchi za Afrika kama Rwanda, Uganda na Cameroon waliorefusha kipindi cha uongozi wa rais au kubadilisha katiba kwa shabaha ya kubakia madarakani.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako