If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Friday, October 5, 2018

Wapinzani wa Burundi walioko uhamishoni kushiriki mazungumzo ya amani ya Arusha, Tanzania

Wapinzani wa Burundi walioko uhamishoni kushiriki mazungumzo ya amani ya Arusha, Tanzania
Wanasiasa wa Burundi wanaoishi uhamishoni wamesema kuwa, wako tayari kushiriki katika mazungumzo ya kusaka suluhu ya mzozo wa Burundi yaliyoitishwa na mpatanishi wa mazungumzo hayo Rais wa zamani wa Tanzania Benjamin William Mkapa kuanzia Oktoba 18 hadi Oktoba 24 mjini Arusha kaskazini mwa Tanzania.

Muungano wa wanasiasa waishio uhamishoni (Cnared) unasema kuwa, utakuwa tayari kushiriki kwenye mazungumzo hayo ambayo hata hivyo yanakosolewa vikali na baadhi ya mashirika ya kiraia ambayo yanasema hayajaona hamu na shauku yoyote kutoka kwa serikali ya Rais Pierre Nkurunziza ya kutaka kumaliza mzozo wa kisiasa unaoikabili nchi hiyo.

Onesime Nduwimana msemaji wa muungano wa vyama vya upinzani (CNARED) anaona itakuwa ni fursa nzuri kuona mazungumzo hayo yanawashirikisha wadau wote katika mgogoro wa Burundi, vinginevyo itakuwa ni kupoteza muda na kwamba Warundi wana matarajio makubwa kutoka kwa wadau wote wa kisiasa.

Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi

Mashirika kadhaa ya kiraia yanaona kuwa mzungumzo hayo yajayo hayatakuwa suluhu ya mzozo uliopo ukizingatia kuwa serikali ya Burundi bado hainaonyesha umuhimu wa kuzungumza na wapinzani wake.


Serikali ya Burundi imekuwa ikipinga kuketi kwenye meza ya mazungumzo na wanasiasa hao kutoka CNARED ikiwashtumu kwamba baadhi yao walihusika katika jaribio la mapinduzi lililotibuliwa Mei 15, 2015.

Burundi ilitumbukia katika machafuko ya kisiasa mapema mwaka 2015 baada ya Rais Pierre Nkurunziza kutangaza kuwa atagombea kiti cha urais kwa muhula mwingine wa tatu; hatua ambayo wapinzani walisema ilikuwa kinyume na katiba ya nchi hiyo.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako