If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Thursday, October 18, 2018

WATAKAOKUMBWA NA MAFURIKO MABONDENI WAJIANDAE ‘KUJIBEBA’

Na HUSSEIN ISSA, Mwananchi, hissa@mwananchi.co.tz DAR ES SALAAM, Tanzania

MAMLAKA ya Hali ya Hewa (TMA) imetahadharisha uwezekano wa kunyesha mvua kubwa hasa katika mikoa ya pwani na Serikali ikiwaonya waishio mabondeni kuwa haitahusika endapo hali hiyo itatokea.

Mafuriko Dar es Salaam
Mafuriko Aprili 2018 jijini Dar es Salaam yamesababisha uharibifu mkubwa kwa familia kadhaa. Juu ni picha ya Profesa Anna Tibaijuka. Picha/MWANANCHI

Mikoa inayopakana na Bahari ya Hindi; Dar es Salaam, Tanga na Pwani imekuwa ikikumbwa na mafuriko hasa katika maeneo ya mabondeni, nyakati za mvua kubwa na utabiri wa TMA unaonyesha hata visiwa vya Unguja na Pemba vinaweza kukumbwa na mvua hizo.

Meneja wa kitengo cha utabiri wa TMA, Samweli Mbuya aliitaja mikoa mingine itakayokumbwa na mvua hizo kubwa za mwezi huu kuwa ni Morogoro pamoja na ya Kanda ya Ziwa; Kagera, Mara Simiyu, Geita, Mwanza na Shinyanga.

Alisema ongezeko la mvua linatokana na uwezekano wa kutokea vimbunga katika eneo la Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi.

“Lakini kesho (leo) Mamlaka ya Hali ya Hewa tutaongea na waandishi wa habari kuhusu mwelekeo wa mvua hizo hapa nchini,’’ alisema Mbuya.

Hata hivyo, kwa mujibu wa tovuti ya mamlaka hiyo, maeneo mengine mengi yatakuwa na mvua za vuli kuwa za wastani.

Vilevile, mvua za juu ya wastani zinatarajiwa katika maeneo ya pwani ya Kaskazini katika kipindi cha msimu wa mvua wa Oktoba hadi Desemba.


Wakati TMA ikisema hayo, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Mussa Sima ameiambia Mwananchi wananchi wote wanaoishi mabondeni wanatakiwa kuondoka haraka kabla hawajakumbwa na madhara.

“Serikali ilishawaambia wahame muda mrefu, sasa labda nirudie tena kuwaambia kuwa waondoke wenyewe kwa sababu mvua zinatarajiwa kuanza kunyesha muda wowote kuanzia sasa na ikiwa watakaidi na kupata matatizo, Serikali haitahusika tena,” alisema Sima.

“Tumeshashuhudia siku zilizopita kuna baadhi ya watu walipata matatizo sana wakiwa bondeni baada ya nyumba zao kubomolewa huku wengine wakipoteza maisha kutokana na mvua hizo.

“(Wakati huo) Serikali ikawahurumia na kuwahamisha kuwapeleka Mabwepande (Dar es Salaam). Lakini sasa wamerudi tena. Narudia kusema wahame.”

Mkurugenzi Dar anasemaje?

Akizungumzia suala hilo, mkurugenzi mtendaji wa Jiji la Dar es Salaam, Siporah Liana alisema kuna tatizo la wapi pa kuwapeleka watu wanaoishi mabondeni, hususan wakati wa mvua.

Alisema uongozi wa jiji utakutana na mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kupanga namna ya kuwahamisha watu wote wanaoishi mabondeni kwa sababu mvua zinakaribia kuanza.

“Ni kweli mvua zinakaribia, sasa kinachofanyika ni kukaa na mkuu wa mkoa (Paul Makonda) kupanga nini cha kufanya kuhusu hawa ndugu zetu,’’ alisema Liana.

Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara aliwataka watu wanaoishi mabondeni kuondoka kabla ya kupata madhara kwa sababu wakitegemea misaada ya Serikali wanaweza kuikosa.

“Wanatakiwa kujiondoa wenyewe kwa sababu mvua ndizo hizo zinakaribia kuanza ili wasipate madhara. Wasidhani kutakuwa na msaada kutoka serikalini,” alisema Waitara.

“Nilishawahi kusikia wanatakiwa kuondoka wenyewe kwa hiari yao, basi na wafanye hivyo wasidhani Serikali inatania inapowataka waondoke.”

No comments:

Post a Comment

Maoni yako