If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Tuesday, November 13, 2018

JPM: SIJALI KUWABADILISHA MAWAZIRI HATA KILA SIKU

Na ELIZABETH EDWARD, Mwananchi/ eedward@mwananchi.co.tz /DAR ES SALAAM, Tanzania

RAIS John Magufuli ameweka wazi msimamo wake kuwa hatasita kufanya mabadiliko ya mara kwa mara kwenye baraza lake la mawaziri endapo ataona mambo hayaendi.

Rais John Magufuli akitoa hotuba
Rais John Magufuli akihutubu awali. Picha/AFP

Akizungumza wakati wa hafla ya kuwaapisha mawaziri wawili na manaibu waziri wanne Jumatatu, Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli alisema hatajali kufanya mabadiliko hata kila baada ya miezi mitano ili mradi mambo yaende sawa.

Kauli yake imekuja baada ya mabadiliko aliyoyafanya wiki iliyopita na kufikisha idadi ya mawaziri tisa aliowaondoa hadi sasa katika baraza la mawaziri aliloanza nalo 2015 alipoingia madarakani.

“Sina tatizo na mtu na wala mimi sio mkorofi, ukiona nakufikia ujue umeshindwa kutekeleza wajibu wako, kila mmoja alikula kiapo cha kuwatumikia wananchi na mwisho akamalizia kusema Mungu nisaidie,” alisema Rais.

“Sitajali kubadilisha kila siku, kwanza Bunge lina wabunge 360 hata wakizunguka wote, ninachotaka ni maendeleo na hilo litawezekana kwa kufanya kazi.”

“Tena leo asubuhi nilikuwa nasoma gazeti moja limenikumbusha kwamba tayari nimeshawaondoa mawaziri tisa na nilianza nao safari hii wamebaki tisa. Sasa najiuliza hadi kumaliza hiyo miaka miwili watabaki wangapi, ila mimi sijali hata nikibaki na mmoja,” alisema Rais Magufuli bila kulitaja gazeti hilo.


Uchambuzi

Hata hivyo, Jumatatu gazeti la Mwananchi katika ukurasa wake wa mbele lilichapisha habari iliyofanyiwa uchambuzi kuhusu mawaziri walioachwa na waliobaki kwenye baraza la mawaziri.

Habari hiyo ilibebwa na kichwa cha habari kilichosomeka “Hakuna aliye salama” na kutaja mawaziri tisa walioshindwa safari ya Magufuli ndani ya miaka mitatu.

Rais Magufuli pia aliwasihi wateule wake kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kutohofia kuchukua hatua pale inapotakiwa. “Mawaziri kachukueni hatua, ni heri mharibu kuliko kukaa kusubiri kazi zenu zifanywe na Waziri Mkuu, mimi sio mkorofi, ni mpole ila usipofanya majukumu yako nitakutoa,” alisema.

“Sikilizeni maelekezo na mengine mtakutana nayo kwa makatibu wakuu, hakikisheni mnasimamia mamlaka na taasisi zifanye kazi zao kama inavyotakiwa, mwisho wa siku Watanzania wanataka maendeleo.”

Aliwatia moyo mawaziri hao kuwa wasihofie changamoto watakazokutana nazo bungeni kwa kuwa anafahamu si wabunge wote watakaowapenda.

Via swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako