If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Thursday, November 15, 2018

Moto waua watu wapatao 60 katika jimbo la California, Marekani

Moto waua watu wapatao 60 katika jimbo la California, Marekani
Maafisa wa jimbo la California nchini Marekani wametangaza kuwa, kutokana na serikali kuu kutochukua hatua za kuudhibiti moto uliozuka kwenye misitu ya jimbo hilo, idadi ya watu walioaga dunia hadi sasa kutokana na moto huo imefikia 59.

Maafisa wa jimbo la California wamesema, wakati moto huo unaendelea kuwaka katika misitu ya jimbo hilo kwa siku ya saba sasa, watu wasiopungua 59 wameshapoteza maisha na wengine zaidi ya 130 hawajulikani waliko.

Sehemu kubwa ya moto huo, unaojulikana kama Camp Fire na ambao unaendelea kuwaka katika sehemu tatu za jimbo la California kwa wakati mmoja, imelikumba eneo la kaskazini ya jimbo hilo.

Kwa mujibu wa maafisa wa jimbo la California, Camp Fire hadi sasa umeshateketeza hekta 137,000 za misitu ya kaskazini mwa jimbo hilo pamoja na nyumba karibu 9,000.

Watu wakifarijiana mbele ya magofu ya nyumba yao iliyoteketea kwa moto

Ripoti zinaeleza kuwa moto huo unaendelea kusambaa na bado haujazimwa.

Moto uliozuka siku ya Alkhamisi iliyopita katika jimbo hilo la California nchini Marekani umesababisha watu 52,000 wabaki bila makazi, wakati hadi sasa maafisa wa jimbo hilo wameweza kuwapatia hifadhi watu wapatao 1,400 tu.

Moto huo mkali umeugeuza jivu tupu mji wa Paradise katika jimbo hilo lililoko magharibi mwa Marekani.../

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako