If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Thursday, December 6, 2018

Sisitizo la Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa UN la kuchunguzwa mauaji ya Kashoggi

Michelle Bachelet
Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amesisitiza ulazima wa kufanyika uchunguzi wa kimataifa ili kutambuliwa mhusika wa mauaji ya mwandishi habari mkosoaji wa utawala wa Aal Saud, Jamal Khashoggi.

Bi Michelle Bachelet amesema kuwa, uchunguzi wa kimataifa unapasa kufanyika ili kumbaini mhusika wa mauaji ya Jamal Khashoggi mwandishi habari mkosoaji wa utawala wa Saudi Arabia. 

Awali Kamisha Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa alitaka kuwekwa wazi taarifa kamili kuhusiana na faili la mauaji ya mwandishi huyo wa habari aliyekuwa akiukosoa utawala wa Aal Saud.

Jamal Khashoggi, mwandishi habari aliyeuawa

Wakati huo huo Sarah Morgan Mkuu wa Ofisi ya shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch mjini Washington ametaka kufanyike uchunguzi wa kimataifa kuhusu mauaji ya Jamal Khashoggi na kusisitiza kwamba faili la mauaji hayo linapaswa kufikishwa katika mahakama ya kimataifa.


Shirika la uujasusi la Marekani (CIA) siku kadhaa zilizopita lilitoa ripoti inayoonyesha kuwa, Muhammad bin Salman ,Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudi Arabia ndiye aliyeamuru kuuliwa Jamal Khashoggi.

Mwandishi huyo wa habari alitoweka tarehe Pili mwezi Oktoba mwaka huu baada ya kuingia katika ubalozi mdogo wa Saudi Arabia mjini Istanbul, Uturuki na siku kadhaa baadaye vyombo vya habari vikatangaza habari kuhusu mauaji ya kutisha ya mwandishi huyo wa habari ndani ya ubalozi huo.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako