If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Tuesday, December 4, 2018

UZURI NA UBAYA WA SIMU ZA MKONONI

Na JOSEPH CHIKAKA

TEKNOLOJIA ya Habari na Mawasiliano (Tehama) kama somo, huwawezesha wanafunzi kuwa na uwezo wa kufahamu na kutumia vifaa vingi vinavyohusiana na teknolojia, habari na mawasiliano.

Samsung Galaxy
Samsung Galaxy. Picha/HISANI

Vifaa hivyo vinaweza kuwa vya kusikia tu kama vile radio; vya kuona kama vile picha, maandishi, michoro ama vinavyomwezesha mtu kuona na kusikia kama vile runinga na sinema.

Kwa mujibu wa mihtasari ya somo la Tehama kwa ngazi ya shule za msingi, yapo malengo kwa kila darasa.

Kwa mfano, wanafunzi hupaswa kujengewa uwezo wa kuandika barua za aina mbalimbali mfano, barua ya kirafiki au kikazi na kutumia runinga, maktaba, kompyuta na intaneti.

Jambo jingine ambalo hufundishwa katika ngazi ya hiyo ya elimu ya msingi ni matumizi simu. Simu ni kifaa mojawapo cha mawasiliano na katika zama hizi zimeboreshwa zaidi na zimepunguzwa ukubwa, hivyo humwezesha mtumiaji kubeba kwa urahisi popote anapotaka kwenda.

Pia, simu hasa za kisasa zimefuata mabadiliko ya mifumo ya kompyuta na zenyewe zimekuwa na uwezo mkubwa.

Hivyo, kwa matumizi hayo simu siyo chombo cha mawasiliano tu ni zaidi ya hapo. Simu zina kamera, redio, skana ya alama maalumu, tochi, hurekodi sauti, video na shughuli nyingine nyingi.

Wanafunzi wengi wa elimu ya juu hususan wa mwaka wa kwanza katika ngazi za diploma na shahada hukabiliwa na changamoto za matumizi ya simu kwa sababu mbalimbali. Tujiulize kwa nini simu zinatumika sana vyuoni?


Moja, ni mabadiliko ya mazingira kutoka katika mfumo wa maisha ya kuwa chini ya uangalizi wa mzazi au walimu. Afikapo chuo kikuu hakuna mtu wa kumlazimisha mwanafunzi kusoma. Mwanafunzi ambaye hakuwa amejengewa hali ya kujitambua hupata shida na mwisho huweza kuharibikiwa kimasomo na kimaisha.

Mbili, kuwa na fedha na kujipangia matumizi yake bila ya kulazimishwa na mtu yeyote. Wanafunzi wengi walipokuwa katika ngazi ya elimu ya sekondari na kushuka chini walikuwa wakilipiwa ada moja kwa moja na wazazi wao, hivyo ni wachache waliozowea kumiliki kiwango kikubwa cha fedha.
Simu za kisasa zinapotumiwa ipasavyo zina faida nyingi kwa wanafunzi wa elimu ya juu na baadhi yake ni hizi.

Mosi, kupashana habari kuhusu mabadiliko ya vipindi. Makundi mengi ya mitandao ya WhatsApp yametumika kufanya mawasiliano na majadiliano na kuafikiana kwa urahisi. Hilo huwalazimisha wanafunzi kuwa na intaneti katika simu zao wakati wote.

Mbili, kufanya marejeo mbalimbali ya masomo yaliyowekwa katika intaneti. Matumizi hayo sahihi huwawezesha wanafunzi wanaotumia mtandao wa picha jongefu kama vile YouTube kupakua video zenye mafunzo mbalimbali kuhusu masomo yao.

Tatu, kufanya uchaguzi wa masomo kupitia njia ya intaneti. Vyuo vingi nchini tayari vimetengeneza kanzidata zenye taarifa za kila mwanafunzi. Kupitia mtandao mwanafunzi huwa na akaunti yake ambayo humwezesha kuona matokeo ya mitihani yake, kuchagua viongozi wa serikali yake ya mwanafunzi na kupokea notisi za walimu wa masomo.

Hata hivyo, wapo wanaotumia simu hizi katika mambo yasiyo na tija na hata kuzitumia vibaya kama vile kuendekeza udaku katika mitandao ya kijamii kuliko kuzingatia masomo. Wanafunzi wengi hujikuta wanatumia muda mwingi kupiga soga, yaani wanaweza kusogoa kwa muda mwingi. Hilo huwagharimu kipindi cha mitihani ambapo hujikuta kuwa na viporo vingi na muda waliupoteza.

Nne, kuiga maisha ya wengine na kuishi maisha ya kinadharia, maisha ya kimtandao yasiyo halisi. Hilo huweza kupunguza umoja na ushirikiano. Wengi hujitengenezea mipaka bila kujitambua kutokana na yale wanayoyarusha mitandaoni.

Matumizi mabaya ya simu hupunguza au kuua ari ya usomaji wa vitabu.

Wanafunzi wengi hudhani kuwa simu na teknolojia zinaweza kuwa mbadala wa vitabu vilivyochapishwa. Kweli, vipo vitabu vingi vinavyoweza kupakuliwa kutoka katika mfumo wa intaneti, lakini haviwezi kuwa mbadala wa machapisho halisi.

Mazoea hayo huzaa tabia ya wanafunzi wengi kukacha kwenda maktaba.

Utamaduni huo huota mizizi na kuhamia katika familia na ofisini ambapo ni watu wachache hufikiri kuwa na makabati ya vitabu au vyumba vya kujisomea.

Nne, kufanya udanganyifu katika chumba cha mitihani. Wapo baadhi ya wanafunzi huingia na simu na kujaribu kutafuta majawabu ya maswali ya mitihani.

Kwa mtazamo wangu suluhu ya mjadala wa simu vyuoni ni kujenga msingi wa matumizi bora ya vifaa vya Tehama tangu wanafunzi wakiwa ngazi za chini.

+255658423258

Chanzo: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako