If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Monday, December 3, 2018

Watu milioni 40 ni waathirika wa utumwa duniani kote

Watu milioni 40 ni waathirika wa utumwa duniani kote
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi Duniani, ILO, linasema utumwa bado ni tatizo kubwa linalowathiri zaidi ya watu milioni 40 duniani kote, watoto wakiwa ni robo ya idadi nzima. Hayo yanajiri pamoja na uwepo wa itifaki ya kuzuia hali hiyo ya kulazimishwa kufanya kazi iliyofikiwa mwaka 2016.

Ripoti ya ILO kuhusu utumwa imetolewa tarehe pili Desemba kwa munasaba wa siku ya Umoja wa Mataifa ya kutokomeza utumwa ikiwa ni kutekeleza azimio lililowekwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tangu mwaka 1951.

Siku hii huwa fursa ya kukuza uelewa kuhusu tatizo la utumwa duniani na kujikita katika kumaliza mifumo mipya ya utumwa kama vile usafirishaji haramu wa watu, ukatili wa kingono, mifumo mibaya ya utumikishaji watoto, ndoa za lazima na utumiaji wa watoto katika migogoro ya kivita.

Taarifa hiyo ya ILO inasema kazi nyingi wanazopewa watoto ni kuwatumia vibaya kiuchumi kinyume na mkataba wa kimataifa wa haki za watoto ambao unatambua haki ya watoto kulindwa dhidi ya kutumiwa vibaya kiuchumi na kutumikishwa katika kazi ambazo zinaweza kuhatarisha maisha yao au kuingilia masomo yao au kuwaumiza kiafya na kimwili, kiimani, kimaadili au maendeleo ya kijamii.

Watoto wanaotumikishwa jeshini kinyume cha sheria za kimataifa

Usafirishaji haramu wa binadamu pia unazuiwa na itifaki ya kuzuia kukandamiza na kusafirisha watu kiharamu hasa wanawake na watoto. Hiyo ni kutokana na mkataba ulioidhinishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa la mwaka 2000, mkataba ambao unasema kuwa usafirishaji haramu wa watu ni kuwachukua watu, kuwasafirisha, kuwahamisha, au kuwapokea kwa mfumo wa kuwatisha au kutumia nguvu au aina nyingine ya matumizi ya nguvu kwa lengo la kupata faida za kiuchumi kinyume cha sheria.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako