Jeneza la Marehemu Mina Said Omari likipelekwa ndani ya msikiti wa Islamic Society uliopo Frederick, Maryland.
Jeneza lililobeba mwili wa Marehemu Mina Said Omari, aliyefariki siku ya Jumatano Sept 21, 2011 saa 4 usiku (10pm) Frederick Memorial Hospital likiwa ndani ya msikiti wa Islamic Society uliopo Frederick, Maryland kwa ajili ya kusaliwa.
Ndugu jamaa na marafiki wakiwa ndani ya msikiti wa Islamic Society uliopo Frederick Maryland
Waumini wa kiislamu wakijitayarisha kwaajili ya sala ya jeneza
Bi Hawa Hemed kutoka Columbus, OH akiwa kwenye msiba wa Marehemu Mina Said Omari.
Waumini wakitoka msikitini baada ya sala ya ijumaa pamoja na sala ya maiti tayari kuelekea makaburi ya Al firdaus Memorial Gardens yaliyopo bara bara ya New Design, Frederick, Maryland.
Mama mzazi wa marehemu Mina Said Omari, watatu kutoka kushoto Bi Zam Zam Maalim Rashid akiwa na Waheeda Margaret Gathesha (kulia) na Mama Raju Tambwe nje ya msikititi wa Islamic Society uliopo Frederick, Maryland nchini Marekani.
Eneo la kaburi alipozikiwa marehemu



Tunamshukuru M/Mungu kwa kufanikisha mazishi ya dada yetu Mpendwa Marehemu Mina Said Omari Mola amjalie Makaazi Meema peponi Insha'Alla Amin
ReplyDeleteAssallam Allykuim ummma wa kiislam
ReplyDeleteNapenda kwanza kumshukuru mola wangu kwa kunipa hatua ya kukamata kalamu na kutoa maoni yangu kuhusu na msiba wa ndugu yetu mpendwa Marehemu mina Said Omar , Mola wetu ametupa roho na uhai na maisha ya katika dunia hii na pia ametupa mauti ambayo hatimaye kifo kwa waja wake kifo cha dada yetu hakika kimetokana kwa uwezo wa allah kareem na hivi sasa amefika mbele ya haki kama wengine waliotangulia mbele yake tunatakiwa kumuombea duwa ili mwenyezi mungu kumuondeshea adahabu ya kaburi na kumpa amali njema ya pepo katika siku ya mkusanyiko wa umma wa kiislam , picha zinazojionesha hapo juu hakika ni mfano halisi ambao kila mmoja hapa katika dunia anaweza kukabiliana na hatima hiyo tunatakiwa waumini wote kujiweka tayari wakati popote bila ya kurudi na mshikamano wetu ndio muhimu katika kujiweka pamoja katika mambo ya misiba ambayo inaweza kutoa hapa Marekani katika majimbo yoyote tumuombe Allah atupe muafaka mwema na kujikusanya tena kwa lolote linaloweza kujitokeza kwa muislam yoyote na wale wote waumini wa dini nyengine kutoka Tanzania umoja wetu hapa Marekani ni mshikamano wa upendo katika kukabiliana na mambo muhimu ya misiba , maradhi na majukumu mengine
Allah atupe afya njema na kutuonesha njia nzuri katika mambo mengine ya kijamii
Wasallam Allykuim
AMIN ALLY
BELLEVUE WA
Mungu amlaze mahali pemapeponi Amina.
ReplyDeleteAmin Amin kwa maneno yako mazuri ya kuweka ukumbusho zaidi kwa jambo hilo kwa ni lamoja tu bali ni letu sote muhimu zaidi tuwe na umoja, ushirikiano,na ustahi wajamii kwani bila ya jamii yetu tuipendayo tusingefanikisha jambo hili kwa kiurahisi na kwa kiimani ya dini yetu. shkran pia dada wa swahili na swahili kwa dua zako Amin
ReplyDelete