If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Saturday, April 21, 2012

SMZ haitakivumilia Kikundi chochote kitakachoonekana kuhatarisha Amani, Utulivu na Umoja wa Visiwa hivi vya Unguja na Pemba.

Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akifunga Mkutano wa Saba wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar huko Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Balozi Seif alitahadharisha kwamba Serikali haitasita kukizuia Kikundi chochote kinachoendesha mihadhara au Makongamano yatakayobainika yanahatarisha usalama wa Nchi.

Alisema Serikali haikatazi Kuendeshwa kwa mihadhara na Makongamano na ndio maana ikavumilia ikidhani kuwa nia ya mihadhara hiyo ni kuelimisha Jamii. Alisema hivi karibuni kipo kikundi kinachoendesha Mihadhara na Makongamano inayotishia hali ya Amani na Utulivu kwa kuhamasisha kwa nguvu watu kuukataa Muungano huku wakitukana kwa nguvu zote Viongozi wa Taifa hili wakiwemo wanaounga Muungano. 

“Mihadhara hiyo imebadilika sura na badala ya kuelimisha imekuwa ni uwanja wa kashfa, kejeli na matusi ya nguoni kwa Viongozi wetu, jambo ambalo ni kinyume kabisa na utamaduni wa Mzanzibari na Misingi ya Kidemokrasia. Kwa hili hatutokuwa na muhali a Mtu wals Kikundi chochote” Alikemea Balozi Seif. Balozi Seif aliwaomba Wananchi kuwa fursa iliyotolewa na Serikali zote mbili kwa kuleta mchakato wa Katiba mpya ni jambo la Kihistoria na linaonyesha kukua kwa Demokrasia Nchini Tanzania. 

Akizungumzia uimarishaji wa Zao la Karafuu Serikali imejiandaa kuhakikisha miche ya Mikarafuu inapatikana katika Vitalu vyake vyote na kwamba wakulima wote Nchini watapatiwa Miche hiyo bila ya malipo. 


Balozi Seif aliwaomba Wakulima na Wananchi wote kuitumia fursa hiyo kwa kuzingatia maelekezo na masharti ya Wataalamu katika utayarishaji wa Mashamba kabla ya kupatiwa michez hiyo. Alisema Karafuu ni Zao Mama na litaendelea kutegemewa kuwa Uchumi wa Zanzibar kwa miaka mingi ijayo. Hivyo katika kutimiza azma ya kuimarisha zao hilo jitihada zitaongezwa kwa lengo la kuongeza kipato cha Wananchi na Taifa kwa Ujumla. 

“ Nawaomba Waheshimiwa wenzangu wanaotoka katika maeneo yanayolimwa Mikarafuu kuichangamkia Miche inayotolewa kwa kuwahamasisha Wananchi katika Majimbo yao kuipanda kwa wingi Miche hiyo” Alisisitiza Balozi Seif. Balozi Seif alifafanua kwamba zao la Karafuu limekabiliwa na ukongwe wa Mikarafuu unaopelekea kuwepo kwa uzalishaji mdogo wa zao hilo. 

Kuhusu suala la Kamati Teule ya Baraza la Wawakilishi Balozi Seif alieleza kwamba Ripoti ya Kamati hiyo imetoa nafasi nyengine kwa Serikali kuona namna ambavyo Baraza hilo limejipanga kuona Serikali inabadilika katika utendaji na uwajibikaji wake. Balozi Seif kwa niaba ya Serikali ameipongeza Kazi nzuri iliyofanywa na Kamati hiyo pamoja na michango iliyotolewa kuhusiana na Ripoti hiyo. 

Alisema Serikali inathamini juhudi hizo za Baraza la Wawakilishi kwa sababu zimeunga mkono kauli mbiu ya Serikali kuwa inaachana na utendaji wa kimazoea { Business as usual }. Kikao cha Baraza la Wawakilishi kimeahirishwa hadi saa 3.00 za asubuhi ya siku ya Jumatano ya Tarahe 13 Juni mwaka huu wa 2012. Othman Khamis Ame Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar 20/4/2012.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako