If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Monday, May 14, 2012

SIMBA YAFUNGWA 'KIUME' NCHINI SUDAN


SIMBA SC imeshindwa kutimiza ndoto za kusonga mbele kwenye Kombe la Shirikisho la Soka Afrika, baada ya kutolewa kwa penalti 9-8 na Al Ahly Shandy ya Sudan kufuatia sare ya jumla ya tatu.

Katika mchezo huo, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shandi, penalti za Shandy zilifungwa na Razak Yakubu, Orwa, Bashir, Saddam, Isaac Seun Malik, Faris Abdallah, Fareed Mohamed Zakaria Nasu na kipa Abdulrahman Ali. Waliofunga penalti za Simba ni Felix Sunzu, Salum Machaku, Emanuel Okwi, Shomari Kapombe, Kelvin Yondan, Victor Costa, Mwinyi Kazimoto na Amir Maftah.


Eltigani alikosa kwa upoande wa Shandy wakati Mafisango na Kaseja walikosa. Aliyeihakikishia Simba kutpolewa alikuwa ni Nahodha Kaseja, ambaye alikosa penalti ya 10. Shandy waliingia kwenye mchezo wa leo, wakiwa nyuma kwa 3-0 kutokana na ujshindi wa SImba kwenye mechi ya kwanza, Dar es Salaam. Hadi mapumziko, hakuna timu iliyokuwa imeona lango la mwenzake na hiyo ilijenga matumaini kwamba, SImba itasonga mbele, lakini kipindi cha pili mambo yalibadilika mno. 

Mabao mawili ya Fareed Mohamed katika za 46 na 64 na lingine la Hamouda Bashir dakika ya 50, yaliisaidia Al Ahly Shandy kushinda 3-0 na kufanya sare ya jumla ya 3-3, baada ya dakika 180 za mechi mbili. Lawama zote zimuendee beki Victor Costa kwa kufungisha mabao mawili- hususan la pili na la tatu ambalo dhahiri yalitokana na ‘ubishoo’ wake usio na maana. Hii inahidhirisha mchezaji huyo aliyepangwa kwa dharula leo, kocha Milovan Cirkovick alikuwa hakosei kutompanga- kwani leo ameigharimu timu na haijulikani kwa nini apangwe yeye badala ya Obadia Mungusa.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako