Maji wa EPIQ BSS wakiwa wamesimama kimya kwa dakika mbili ili kutoa heshima kwa watu waliopoteza maisha katika ajali ya Boti ya MV Skagit iliyozama juzi huko Zanzibar kabla ya kuazan kwa usaili wa vijana watakao shiriki shindano hilo kutoka Mkoani Mbeya ambapo zoezi linafanyika kwa siku mbili Julai 21-22, 2012 katika ukumbi wa CLUB VYBES mjini Mbeya. Majaji hao kutoka kushoto ni Salama Jabir, Madam Ritha, Masta J na Meneja Mawasilino wa Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel, Awaichi Mawala.
Vijana kibao wa mjini Mbeya wamejitokeza kuwania nafasi ya kuwakilisha mkoa huo katika shindano la EPIQ BSS mjini Mbeya na hapa ni vijana waliofika Club Vybes katika usaili wakibandika namba zao.
Baadhi ya washiriki waliojitokeza katika usaili huo wakiwasikiliza maelekezo kutoka kwa wasimamizi kabla ya kwenda mbele ya majaji.



No comments:
Post a Comment