If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Wednesday, August 22, 2012

IKULU:Rais Jakaya Kikwete Aomboleza Kifo Cha Waziri Mkuu wa Ethiopia

Rais Jakaya Kikwete, Marehemu Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mheshimiwa Meles Zenawi,

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete asubuhi ya jana, Jumanne, Agosti 21, 2012, amepokea kwa mshtuko mkubwa, masikitiko na huzuni nyingi taarifa za kifo cha Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mheshimiwa Meles Zenawi, kilichotokea jana usiku nje ya nchi ambako alikuwa anatibiwa.

Kufuatia taarifa hizo, Mheshimiwa Rais Kikwete, kwa niaba ya wananchi wa Tanzania, Serikali yake na kwa niaba yake mwenyewe amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Ethiopia, Mheshimiwa Girma Wolde-Giorgis.

Katika rambirambi zake kwa Mheshimiwa Wolde-Georgis, Rais Kikwete amesema: “Tanzania imepokea kwa mshtuko mkubwa, masikitiko na huzuni nyingi taarifa za kifo cha Mheshimiwa Meles Zenawi kilichotokea jana usiku.”

Amesema Rais Kikwete: “Kwa niaba ya wananchi wa Tanzania, Serikali yangu na mimi mwenyewe, natuma salamu zangu za dhati za rambirambi kwako, kwa wananchi wa Ethiopia na kupitia kwako kwa Mheshimiwa Azeb Mesfin, mjane wa marehemu na familia nzima ya Mheshimiwa Meles Zenawi. Tupo nanyi katika msiba huu mkubwa.”

“Kwa hakika, Ethiopia imempoteza kiongozi hodari, mwana mapinduzi na mpenda maendeleo. Kwa hakika, Afrika imempoteza kiongozi wa kutumainiwa na msemaji hodari sana wa Bara letu. Daima tutamkumbuka Waziri Mkuu Zenawi kwa msimamo wake thabiti wa kutetea maslahi ya Afrika na ustawi wa watu wake. Mimi na Tanzania tumempoteza rafiki wa kweli” amesema Rais Kikwete na kusisitiza, “hakika tutaukosa mchango wake uliojaa busara, hoja zake za kusisimua na zenye mantiki sana.”

Rais Kikwete amemaliza kwa kuwaeleza wananchi wa Ethiopia: “Tunaungana nanyi katika wakati huu mgumu wa majonzi na tunamwomba Mwenyeji Mungu awape nguvu, moyo, subira na baraka zake ili muweze kuvuka kipindi hiki. Aidha, tunaungana nanyi na familia ya Marehemu Zenawi kumwomba Mola ampe mapumziko mema Marehemu Meles Zenawi.”

Waziri Mkuu Zenawi ambaye ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 57 amekuwa Waziri Mkuu wa Ethiopia tokea 1995 na kabla ya hapo alikuwa Rais wa nchi hiyo kati ya 1991 na 1995.

Imetolewa na: Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu. Dar es Salaam.
21 Agosti, 2012
Email This. BlogThis!
Share to Twitter
Share to Facebook

1 comment:

  1. Salaam za rambi rambi hazitoshi afanye aende kumzika...

    ReplyDelete

Maoni yako