Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete amesema wakati umefika kwa Halmashauri za Wilaya Tanzania Bara na Zanzibar lazima zilenge kujiandaa vyema katika kufanikisha miradi ya maendeleo iliyobuniwa na hatimae kuanzishwa Wananchi wenyewe katika maeneo yao.
.jpg)
Rais Kikwete akiangalia bidhaa za moja ya banda la miradi ya wajasiri amani iliyoanzishwa katika awamu ya pili ya mradi wa Tasaf nchini Tanzania hapo uwanja wa michezo wa Jamuhuri Mjini Dodoma. Kushoto yake ni Spika wa Bunge Mh. Anna Makinda na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibarf Balozi Seif Ali Iddi .
Dr. Kiwete alitoa agizo hilo wakati wa sherehe za uzinduzi wa Mradi wa Maendeleo ya Jamii Tanzania { Tasaf } awamu ya tatu zilizofanyika katika Uwanja wa Michezo wa Jamuhuri Mjini Dodoma.
Dr. Kiwete alitoa agizo hilo wakati wa sherehe za uzinduzi wa Mradi wa Maendeleo ya Jamii Tanzania { Tasaf } awamu ya tatu zilizofanyika katika Uwanja wa Michezo wa Jamuhuri Mjini Dodoma.
Rais Kikwete alisema ipo miradi mingi iliyoanzishwa na Wananchi na kukamilika akaitolea mfano ile ya Majengo ya Vituo vya Afya na Maskuli lakini hadi sasa inashindwa kutoa huduma zinazostahiki kutokana na sababu ya ukosefu wa watendaji walioatayarishwa na Halmashauri husika.
Alisema utaratibu huo ukipuuzwa kwa kiasi kikubwa unaweza kupunguza ari ya Wananchi ya kubuni miradi itakayowaletea faida yao kiuchumi pamoja na kijamii kwa nia ya kupunguza umaskini.
“ Tumeshuhudia katika baadhi ya Halmashauri zetu zimekuwa na majengo ya Skuli na Vituo vya Afya vilivyokosa kutoa huduma kutokana na Viongozi wa Halmashauri wa Wilaya kuipa kisogo miradi hiyo ya Wananchi kwa vile haikuwa chaguao lao”. Alifafanua Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.
Hata hivyo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ameahidi kwamba Serikali itatumia nguvu zake zote ili kuona miradi iliyoanzishwa kwa nguvu za Wananchi inamalizwa na kutoa hudma zinazokusudiwa.
Aliipongeza Kamati ya Taifa ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania { Tasaf } hatua zake lizochukuwa na kupelekea mafanikio makubwa ndani ya awamu mbili za mradi wa Tasaf Nchini. Dr. Kikwete alisema siri ya Mfanikio ya mradi huo inatokana na ushirikiano a karibu kati ya Kamati, Viongozi wa Wilaya pamoja na Wananchi wenyewer ambao ndio walengwa wa mfuko huo.
Akizungumzia Awamu ya Tatu ya Tasaf Rais Kikwete alisema maandalizi yanafanyika ili mpango huu wa awamu ya tatu uenee nchi nzima kwa kulenga kutolewa mafunzo kwa wananchi pamoja na kuelekezwa vizuri kwa nia ya kuondoa mapungufu yaliyojichomoza katika awamu mbili za mwanzo.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano alieleza kwamba Serikali ina matumaini makubwa kwa awamu ya tatu kufanikiwa nyema kwa vile miekusudia kupunguza umaskini uliokithiri miongoni mwa Jamii hapa Nchini. “ Nimefarajika kuona uwiano wa Kijinsia ndani ya uongozi na miradi yote ya Tasaf umezingatiwa vyema.Ukona vinaelea vimeundwa, hivi ndivyo ilivyo Tasaf”. Dr. Kikwete aliifyagilia Tasaf.
Aliwapongeza washirika wa Maendeleo nje ya nchi hasa ile Benki ya Dunia kwa sera zao zilizobadilika ambazo hivi sasa zinakwenda sambamba katika kutoa msukumo kwenye miradi iliyoanzishwa na Wananchi wenyewe.
Alisema yapo mabadiliko makubwa kwa Taasisi hizo za nje kujiepusha na ile tabia iliyojengeka siku za nyuma ya kuzichagulia Nchi na Wananchi miradi inayozitaka taasisi hizo. “ Tunafurahishwa sana na Sera zao zinazoangaliamiradi iliyopewamsukumo na Wananchi pamoja na Serikali na wao kuwezesha kifedha na Taaluma”.
Kwa hili inafaa wapongezwe, alisisitiza Dr. Kikwete. Mapema Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania Nd. Slaus Mahanga alisema jumla ya miradi 11,572 ilianzishwa na kusimamiwa katika halmashauri zote Nchini Bara na Zanzibar. Nd. Mahanga alisema kati ya miradi hiyo 5875 ilijumuisha kundi kuba la Vijana wasio na ajira pamoja na wanawake wajane wakati 5,435 ililenga katika ujenzi wa madarasapamoja na Vijana anaoishi na virusi vya kimwi wapatao 52,316 walipatia huduma za uwezeshaji kimaisha.
Akitoa salamu za Benki ya Dunia ambayo ndio mfadhili mkuu wa mradi wa Tasaf Meneja wa Benki hiyo Bwana Jack Mosuu alisema uzinduzi wa maradi wa Tasaf ni Historia kwa Tanzania katika harakati zake za kupambana na umaskini kwa Wananchi wake.
Bwana Jack alisema katika kuunga mkono juhudi hizo za Tanzania licha ya changamoto inazopambana nazo lakini Benki hiyo imetenga kutoa Dola za Kimarekani Milioni 250 kusaidia mradi huo ambapo tayari saini kwa ajili ya mpango huo imeshatiwa hivi karibuni.
Akimkaribisha Mgeni rasmi atika uzinduzi wa mradi huo wa Tasaf awamu ya tatu Waziri wan chi Ofisi ya Rais anayesimamia Uratibu na Mahusiano Mh. Seteven Wasira alisema Tasaf imeanzishwa ili kuwawezesha Wananchi wawe na uwezo wa kujitegemea.
Mh. Wasira alisema Tasaf ya awamu ya tatu imepangwa kuwa na sehemu nne muhimu ikiwemo ile muhimu ya Mpango wa Taifa wa kunusuru kaya maskini zilizo katika mazingira hatarishi. Alisisiiza kwamba mgao wa fedha za uwezeshaji kaika awamu hii utazingatia zaidi kwa zile kaya maskini kabisa.



No comments:
Post a Comment