Mambo Matatu Yanayofuatia Ramadhaan: Zakaatul-Fitwr, 'Iydul-Fitwr Na Swawm Ya Sittatush Shawwaal
Tunakaribia kumaliza mwezi Mtukufu wa Ramadhaan na mambo matatu yafuatayo ya muhimu yanayotukabili yanapasa kuzingatiwa ili tukamilishe Swawm zetu ipasavyo na tupate fadhila zake.
1- ZAKAATUL-FITWR
Inaitwa Zakaatul-Fitwr (Zakaah ya Kufuturu au Kufutari) kutokana na kumalizika Swawm ya Ramadhaan. Imefaridhiwa mwaka wa pili wa Hijrah katika mwezi wa Ramadhaan.
Hikma Yake
Ni kutwaharisha Swawm ya Muislamu kutokana na maneno machafu, ya upuuzi wakati alipokuwa amefunga kwa kulisha maskini chakula ili nao wapate chakula kizuri siku ya ‘Iyd. Ndio maana kutolewa kwake kunakuwa kabla ya kuswali Swalaah ya ‘Iydul-Fitwr. Dalili ifuatayo inathibitisha:
Endelea kusoma Alhidaaya.com



No comments:
Post a Comment