If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Wednesday, August 15, 2012

Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa wataka serikali ya Somalia kudhibiti mauaji

Ofisi ya Siasa ya Umoja wa Mataifa kwa Somalia (UNPOS) na Umoja wa Afrika hapo Jumatatu (tarehe 13 Agosti) zimeitaka serikali ya Somalia kuchukua hatua kali dhidi ya wimbi la mauaji yanayowalenga waandishi wa habari, maafisa wa serikali na wafanyabiashara mjini Mogadishu.

Ulinzi umeimarika mjini Mogadishu katika kipindi cha mwaka mmoja lakini mauaji yameongezeka, kwa mujibu wa Kikosi cha Amani ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM).

Watu wenye silaha wasiojulikana wamewaua kwa uchache watu saba ndani ya kipindi cha wiki moja iliyopita, wakiwemo wafanyabiashara na waandishi wa habari, alisema mwakilishi maalum wa Umoja wa Afrika kwa Somalia, Boubacar Diarra.

"Mamlaka za Somalia lazima zifanye uchunguzi kwa mauaji haya kwa mtazamo wa kuwafikisha watendaji wa uhalifu huu wa kinyama kwenye mkono wa sheria," alisema Diarra. "AMISOM iko tayari kutoa msaada wowote inaoweza kusaidia uchunguzi kama huo."


Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Somalia, Augustine Mahiga, alisema: "Haikubaliki kabisa kwamba ndani ya mwaka mmoja mzima, haki haikutendeka kwa wahanga wa uhalifu huu."

Kauli hizi zinafuatia mauaji ya waandishi wa habari, Yusuf Ali Osman na Mohamud Beneyste siku ya Jumapili. Hadi sasa kwa mwaka huu, kwa uchache kila mwezi mwandishi mmoja wa habari amelengwa na kuuawa.

UNPOS iliitaka serikali ya Somalia kuanzisha uchunguzi katika mauaji hayo na ya hivi karibuni. "Utamaduni huu wa kutenda makosa bila kufikishwa kwenye vyombo vya sheria lazima umalizike. Hatupaswi kuruhusu misingi muhimu ya uhuru inayowakilishwa na uhuru wa habari ivunjwe na wale wanaokusudia kutumia vurugu kufikia malengo yao binafsi," alisema Mahiga.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako