If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Friday, August 24, 2012

UN yatembelea vijana kuwahamasisha kuwa wajasiriamali ili kupunguza umasikini.‏

Bi. Harriet Macha (Picha ya kwanza) kutoka Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) akizungumza na mtandao wa vikundi vya vijana kata ya Kibada -Kigamboni akiwaeleza jinsi Umoja wa Mataifa unavyohusika katika maendeleo ya vijana ikiwemo kuwaelimisha haki zao, kuwawezesha kujitambua na kujua umuhimu na kazi za mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini.

  
(Picha ya pili) Naibu Mwenyekiti wa kikundi cha vijana kata ya Kibada akizungumzia changamoto zinazowakabili kama kikundi ikiwemo ukosefu wa maktaba ambazo zingewawezesha kusoma na kujua mashirika hayo yanafanyaje. Pia tatizo lingine ni jeshi la polisi kuwafikiria na sheria zake ikiwemo kuwapangia muda wa kutembea, kukithiriri kwa rushwa mambo ambayo yanachangia kuongeza uduni wa maisha ya vijana.

Mmoja wa mwanakikundi wa vijana kata ya Kibada-Kigamboni mwenye kipaji cha kuigiza akionyesha uwezo wake wa kuigiza ikiwemo jinsi vijana wanavyokwamishwa kuanzia kwenye sekta ya elimu na kujiajiri na hata hivyo Bi. Harriet Macha wa UNIC alitoa ushauri jinsi ambavyo Shirika hilo linavyofanya kazi na serikali na mipaka yake.

Mwanakikundi wa kata ya Kibada Kigamboni akielezea kipaji chake cha ususi kilichompelekea kujiajiri na kujitegemea na kuahidi kutoa mafunzo kwa wasichana wenzake.

Pichani Juu na Chini ni Bi. Harriet Macha kutoka Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) akizungumza na vijana Somangile-Kigamboni kutoka kikundi cha 'Kigamboni Peer Educator Network' (KIPENET) kuhusiana na kazi za shirika hilo na huku akipokea changamoto kutoka kwao.

Angalia zaidi taswira ya habari hii http://dewjiblog.com/

No comments:

Post a Comment

Maoni yako