If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Wednesday, August 15, 2012

ZAIDI YA WATOTO 1500 WANUFAIKA NA VF-RAMADHAN CARE & SHARE

Mkuu kitengo cha Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule akiwakabidhi baadhi ya watoto yatima mbuzi kwa niaba ya watoto wenzao wa mkoa wa Kigoma,wakati wa hafla fupi ya kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali,kupitia kampeni ya Ramadhan Care & Share inaendeshwa na mfuko huo,wakati wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Kaimu Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Kigoma,Shekhe Hassan Idd Hassan Kaburwa,akimkabidhi msaada wa Madaftari mtoto yatima ambae anasoma kidato cha kwanza Zulpha Ally, wakati wa hafla fupi ya kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali,kupitia kampeni ya Ramadhan Care & Share mjini Kigoma inayoendeshwa na Vodacom Foundation,wakati huu wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,wanaoshuhudia kulia ni Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule.

Mkuu kitengo cha Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule akiwanawisha maji baadhi ya watoto yatima wa mkoa wa Kigoma kwa ajili ya kuanza kufuturu na watoto wenzao wa mkoa wa huo,wakati wa hafla fupi ya kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali,kupitia kampeni ya Ramadhan Care & Share inaendeshwa na mfuko huo,wakati wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Meneja wa Vodacom Foundation Bi.Grace Lyon akiwa na mtoto anaeshi katika mazingira magumu Zulpha Ally wakati wa hafla fupi ya kufuturu na kukabidhiwa misaada mbalimbali mkoani Kigoma kwa watoto yatima iliyoandaliwa na Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Ramadhan Care & Share.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako